Kuna kipindi nashikwa na hasira sana nikiwaza yanayoendelea, hivi kwanini wabunge wengi wa CCM wameamua kuwa hivi???? Ni jana tu asubuhi niliona wabunge wa upinzani na wa ccm wakimshangilia JK pamoja, kama hiyo haitoshi jioni yake wabunge wa upinzani wamepiga kura kuchagua wawakilishi kutoka ccm pasipo kuharibu kura, lakini wenzao wakapiga kura za hapana, hivi unataka niamini yule dada mrembo aliyepata kura nyingi anawazidi Ezekia na Masha???? Kwanza ilitakiwa mjue Ezekia na masha ni wapinzani tu hapa tanzania, nje ya hapo mapambano yao ni kutetea maslahi ya Taifa, uwezo wao tunaujua............leo unampeleka mtu kwa kigezo cha urembo aende kupiga selfie au akawalainishe wawakilishi kutoka Rwanda???? Sote tunajua kuwa Rwanda kuna warembo wengi tu, lakini wameamua kupeleka watu wenye uzoefu wanaojua cha kufanya........ inatia hasira sana kwakweli na inavunja moyo sana, nina hakika kama chadema wangemuongeza Wema Sepetu pale basi kura zote zingekua ni NDIYO!!!! Anayway acha tu niishie hapa, nilitaka tu kuwashauri CHADEMA wasiende mahakamani wamuongeze tu Wema pale, then atakaye kwenda naye atamfundisha kama Amina Chifupa (R.I.P) alivyofundishika.......! Otherwise, andaeni strategies nzuri kushinda huu mkakati.