Pre GE2025 CHADEMA Mara: Mbowe akikataa ushauri tutakutana kwenye Sanduku la Kura, waenda na Lissu na Heche

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,671
4,490
Kama ni mpira ball possession team mbowe imezidiwa na team lissu, rafu zinachezwa ile mbaya. Mpira una matokeo ya kikatili team mbowe inaweza kushinda hata kwa mbinu chafu
 

Attachments

  • 5900516-2dae5c1f3887d759229713b8a563fcc1.mp4
    7.1 MB
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka mkoa wa Mara wamejitokeza hadharani na kueleza msimamo wao kuwa kwenye mchakato wa kinyang'anyiro cha kutafuta viongozi wa Kitaifa wa chama hicho wao wanaenda na Tundu Lissu kwa nafasi ya Mwenyekiti na John Heche kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara
View attachment 3194181

Pia, Soma:
Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA

BAWACHA Mbeya wamuunga mkono Lissu
Uchaguzi ulisha isha ,mliochukua vibunda upande ule rudisha mapema sana ,msije sema hatukuwambia
 
Kwa hesabu ya haraka uungwaji mkono wa Mbowe NI mdogo sana atabaki na wajumbe wa Dar, (hapa watagawa Kura) , Arusha, Manyara, Kilimanjaro Mbowe atabeba zote , mikoa iliyobaki ni kama Mbowe kashapoteza mvuto sana
 
Inafika wakati mpaka namuonea huruma ndugu yako Mbowe anavyodhalilika. Alishindwa kusoma upepo na kutanguliza hekma.
Kabla ya kumuonea huruma Mbowe, jionee huruma wewe mwenyewe. Unachoshindwa kuelewa ni kuwa hata kama atashindwa, atakuwa ameonyesha ukomavu wa demokrasia ndani ya chama chake. Ataweza sasa kukaa na kuendelea na biashara zake bila stress za kuongoza chama cha upinzani. Maisha yake yatakuwa mazuri tu. Hauna haja ya kumuonea huruma.

Amandla...
 

Viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka mkoa wa Mara wamejitokeza hadharani na kueleza msimamo wao kuwa kwenye mchakato wa kinyang'anyiro cha kutafuta viongozi wa Kitaifa wa chama hicho wao wanaenda na Tundu Lissu kwa nafasi ya Mwenyekiti na John Heche kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara,

Mbowe nadhani anapashwa kujitoa muda bado anao kwa busara.
 
Back
Top Bottom