Moja ya hoja za kitoto zilizowahi kuletwa na wapinzani ni hii hoja ya kumuondoa Naibu Spika!
Je Chadema inatuambia kuwa Spika Ndugai...mwenyekiti Zungu au Mwenyekiti Chenge ni bora kuliko Naibu Spika?
Je Chadema inatuambia kuwa Naibu Spika akiondolewa atapatikana Naibu Spika 'dhaifu' au muadilifu kutoka CCM?
Je Chadema inatuhakikishia kuwa upinzani ulioko bungeni au bunge kwa ujumla wake litaweza kumchagua Naibu Spika wanaomtaka au atakayekidhi viwango wanavyovitaka ??
Hebu Chadema wawe wakweli waache Siasa za mzaha katika zama hizi za weledi na ukweli.
Fursa ya kukata rufaa ipo lakini hawaitumii huu unaitwa usanii wa hali ya juu.