CHADEMA inatarajia kukusanya kiasi gani cha fedha katika mkakati wake wa kuichangia kidigitali kampeni ya tone tone mpaka kufikia oct. Mwaka huu 2025?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
26,587
26,466
Au ni mpango wa kanyaga twende bora liende tu, na kwamba tone tone ni mpango wa kukusasanya pesa kwaajili ya matumizi ya chama, viongozi waandamizi na familia zao, kwa makusudi ya kazi ya kujitenga au kususia uchaguzi, maandamano na michakato yoyote ya kidemokrasia nchini?

Je, kampeni ya tone tone ni mpango wa mchongo, usio na lengo maalumu la jumla ya kiasi cha fedha zinazotarajiwa kuchangiwa, wala hakuna ukomo wa muda wa kuchangia pesa hizo?

Na,
kwa mantiki hiyo, kampeni ya tone tone sio kichaka cha upigaji pesa kwa machekbob wà mjini wasio na ajira, kutapeli wananchi kidigitali?

Au wewe kama mdau wa siasa,
unaona ni sahihi kwa ukusanyaji wa pesa wa chadema, bila kua na lengo maalumu la ukwasi wanao tarajia kukusasanya, wala ukomo wa muda wa kuchangia ukwasi huo?

Au Chadema imekua nyumba ya ibada ambayo inakusanya sadaka ambayo ni hiyari ya waamini?

Mpaka sasa unadhani wamekusanya kiasi gani kama unafahamu, maana mwanzoni mwa uchangiaji kuliahidiwa uwazi wa kiwango cha juu sana kuhusu kampeni hii, ila hivi sasa kuna usiri mno kwenye kutangaza kiwango kilichokusanywa?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom