Pre GE2025 Chadema inatakiwa kuhamasisha wananchi kwa wingi waende kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Boston12

Member
Feb 23, 2025
79
194
Kwanza ieleweke Mimi ni mfuasi kabisa wa kauli mbiu ya "NO REFORMS NO ELECTION" ila baada ya kuutafakali mstakabali wa taifa letu nimejiridhisha kabisa kwamba CHADEMA inabidi tuanze maandalizi na kuingia rasmi kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Kwa nini nasema hivyo; ni kwa sababu CCM Haina malengo wala uchungu dhidi ya taifa hili hasa Tanganyika.
Na lengo la ccm nikuona CHADEMA ili isishiriki uchaguzi huu na iweze kujitangazia ushindi mkubwa mapema sana.

Sasa mpango uliopo ni kushawishi vyama vidogo vya upinzani nchini vishiriki uchaguzi wa 2025. Na kwa baadhi ya majimbo watawapa wabunge wakutosha ili uchaguzi uonekane umekuwa wa uhuru na haki kwa sababu wabunge na madiwani wa upinzani watapitishwa kwa wingi ili kuzima macho ya kimataifa. Baada ya hapo utaratibu wa wizi na kuhujumu taifa hili utaendelea kwa Kasi ya ajabu.

Sasa kwa lengo la kuharibu mipango hii miovu ya chama kile chakavu, nakiomba chonde chonde CHADEMA tuingie mzigoni kupambana na chama hiki support ya wananchi ni kubwa sana kwa sababu hali ya maisha kwa wananchi yamekuwa magumu sana.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Hakuna reforms zitazotufata tukiwa tumekaa TU bila kushinikiza. Kipindi Cha uchaguzi ndipo jamii huwa umechafukwa kupata mabadiliko yoyote Yale hasa kukifurumusha chama dhalimu.

Kitu ambacho CHADEMA inatakiwa kufanya hivi Sasa ni KUHAMASISHA WANANCHI KWA WINGI WAENDE KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA.

Jambo la pili michakato ya kupata majina mazito Kila Jimbo na kata yaanze kuchakatwa ili twende kwenye uchaguzi tukiwa na watu sahihi wa kushinda majimbo na udiwani na hata urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Jambo litakalo leta mabadiliko kwenye nchi hii ni kupitia wananchi wenye nchi wenyewe pale watakapoelemishwa juu ya kuwa ngangari na kulinda kura zao kwenye vituo vya kupigia kura.

Wananchi wakisimama wenyewe kulinda mabox ya kura, chama kile ni waoga sana ndio maana hutumia vyombo vya usalama. Ila awamu hii wamefeli kwa sababu hata hivyo vyombo vya usalama vinataka haki itawale nchi hii ili kuleta mstakabali ulio Bora kwa vizazi vya Sasa na vijavyo vya taifa la TANZANIA.
 
Its too late man,

Nadhani kufikia sasa tume imeshapita karibia kwenye mikoa yote kuandikisha watu

Na walioenda kujiandikisha 90 percent ni CCM na watu wanaotaka vitambulisho tu

Hata reforms zikifanyika bado CHADEMA wanaenda kuangukia pua kwenye uchaguzi huu
 
Unaijua CCM? Ni Mbunge gan wa CCM atakubali NEC imnyakulie Tonge la Ugali? .

Hivo Vyama vingine vidogovidogo, havina Wagombea wowote wale ambao wanaweza shinda uchaguzi ngazi ya udiwan wala Ubunge, hawana Mgombea wa kushinda CCM Kwa ngazi hizo.

Hivo CCM wakiacha majimbo hayo, kitakua ni kituko Cha mwakaaaaa .

Wewe unaamini Mgombea wa UDP , TADEA, CHAUSTA, DP, NRA, SAU, CCK, UPDP , unadhan , Kuna Mgombea wa kuyumbisha CCM?.

CCM inahitaji uwepo wa CHADEMA au ACT ili kuhalalisha Uchafuzi wa Kura.

No Reforms, No Election
 
Kwanza ieleweke Mimi ni mfuasi kabisa wa kauli mbiu ya "NO REFORMS NO ELECTION" ila baada ya kuutafakali mstakabali wa taifa letu nimejiridhisha kabisa kwamba CHADEMA inabidi tuanze maandalizi na kuingia rasmi kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Kwa nini nasema hivyo; ni kwa sababu CCM Haina malengo wala uchungu dhidi ya taifa hili hasa Tanganyika.
Na lengo la ccm nikuona CHADEMA ili isishiriki uchaguzi huu na iweze kujitangazia ushindi mkubwa mapema sana.

Sasa mpango uliopo ni kushawishi vyama vidogo vya upinzani nchini vishiriki uchaguzi wa 2025. Na kwa baadhi ya majimbo watawapa wabunge wakutosha ili uchaguzi uonekane umekuwa wa uhuru na haki kwa sababu wabunge na madiwani wa upinzani watapitishwa kwa wingi ili kuzima macho ya kimataifa. Baada ya hapo utaratibu wa wizi na kuhujumu taifa hili utaendelea kwa Kasi ya ajabu.

Sasa kwa lengo la kuharibu mipango hii miovu ya chama kile chakavu, nakiomba chonde chonde CHADEMA tuingie mzigoni kupambana na chama hiki support ya wananchi ni kubwa sana kwa sababu hali ya maisha kwa wananchi yamekuwa magumu sana.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Hakuna reforms zitazotufata tukiwa tumekaa TU bila kushinikiza. Kipindi Cha uchaguzi ndipo jamii huwa umechafukwa kupata mabadiliko yoyote Yale hasa kukifurumusha chama dhalimu.

Kitu ambacho CHADEMA inatakiwa kufanya hivi Sasa ni KUHAMASISHA WANANCHI KWA WINGI WAENDE KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA.

Jambo la pili michakato ya kupata majina mazito Kila Jimbo na kata yaanze kuchakatwa ili twende kwenye uchaguzi tukiwa na watu sahihi wa kushinda majimbo na udiwani na hata urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Jambo litakalo leta mabadiliko kwenye nchi hii ni kupitia wananchi wenye nchi wenyewe pale watakapoelemishwa juu ya kuwa ngangari na kulinda kura zao kwenye vituo vya kupigia kura.

Wananchi wakisimama wenyewe kulinda mabox ya kura, chama kile ni waoga sana ndio maana hutumia vyombo vya usalama. Ila awamu hii wamefeli kwa sababu hata hivyo vyombo vya usalama vinataka haki itawale nchi hii ili kuleta mstakabali ulio Bora kwa vizazi vya Sasa na vijavyo vya taifa la TANZANIA.
Yaani kwa maana hiyo unataka kwenda kinyume na Lissu? Ngoja uje ufukuzwe huko! Hujui Chadema na Lissu ni sawa na Korea Kaskazini na Kim jong Un? Shauri yako!
 
Ila awamu hii wamefeli kwa sababu hata hivyo vyombo vya usalama vinataka haki itawale nchi hii ili kuleta mstakabali ulio Bora kwa vizazi vya Sasa na vijavyo vya taifa la TANZANIA
Nakuunga mkono, ila hapa kwenye usalama sio kweli
 
Chadema wakistuka Lissu ni kitengo, na anafanya kazi ya CCM na kitengo kudhoofisha nguvu ya upinzani, itakuwa tuu late, na tutakuwa tumeshamwapisha Mama.

Sasa hivi chadema wanakunywa pombe tu, hawajiandikishi. Lissu kasaidia kuvunja morali
 
Its too late man,

Nadhani kufikia sasa tume imeshapita karibia kwenye mikoa yote kuandikisha watu

Na walioenda kujiandikisha 90 percent ni CCM na watu wanaotaka vitambulisho tu

Hata reforms zikifanyika bado CHADEMA wanaenda kuangukia pua kwenye uchaguzi huu
Unaamini vipi kwamba wote waliojiandikisha watapigia kura ccm pekee?
 
Back
Top Bottom