Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,846
- 39,580
Pamoja na CCM kuwa chama dhaifu kinachotegemea dola na uhalifu kufanya siasa zake, lakini tena bado CHADEMA imekipasua chama hicho kati kwa kati.
Mwaka 1995 wakati NCCR - Mageuzi kilipokuwa maarufu na kila mtu akiamini kwamba chama hicho kitakuja kuwa kikubwa na imara kwenye siasa za Tanzania , Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikuwa na maoni tofauti.
Kwanza Mwalimu alisema NCCR-siyo chama imara ila kinatumia umaarufu wa aliyekuwa kiongozi wa chama hicho Augustine Lyatonga Mrema kufanya siasa zake.
Mwalimu alisema kuwa chama kitakachokuja kuwa Imara ni Chama Cha Maendeleo na Demokrasia - CHADEMA. Leo miaka 30 baadae, maono ya Mwalimu yametimia.
Kutokana na uimara wa CHADEMA, chama hicho kimeipasua CCM kati kwa kati na kutoka makundi mawili yanayopingana yanayobadili msimamo na mitizamo kutokana na wakati.
Kuna kundi kutokana na nyakati, huona CHADEMA ni chama chenye manufaa katika kuijenga nchi yetu kidemokrasia na kuzifanya taasisi za dola ziwe imara.
Lakini Kuna kundi jingine huona kuwa uimara wa CHADEMA ni jambo hatari Sana kwa maslahi yao yanayotokana na CCM kuwepo madarakani.
Harakati hizo za wana CCM ndizo zilizowagawanya kwenye mitizamo yao kuhusu uchaguzi ndani ya CHADEMA mwaka huu.
Kundi linalotaka CHADEMA iwe imara ni lile linalotaka Mwenyekiti wao asiwe Samia Suluhu Hassan, na kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025, wana CCM wengine nao waruhusiwe kugombea nafasi ya Urais kupitia chama hicho.
Kundi linaloombea CHADEMA iparaganyike (kusambaratika haiwezi kutokea), ni lile kundi linalofaidika kwa Samia kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama chao, na Samia kuwa pia mgombea pekee wa Urais kupitia CCM bila kupingwa.
CHADEMA inaamua siasa za nchi hii.