Kuelekea 2025 CHADEMA ifanye mapinduzi ya ndani kwanza ili kuing'oa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,381
6,945
Kweli. Program ya uamsho ifanywe nchi nzima na chadema ili wananchi watoke usingizini.

..sio sahihi kusubiri Chadema watufanyie lila kitu.

..wananchi wenyewe tunaweza kuhamasishana kupigia kura chama tofauti na Ccm.
 
Kwanza kabisa ni kuwag'oa viongozi wenye vinasaba na CCM kama Mbowe na Mnyika.

Pili ni kuleta mabadiliko makubwa kwa kuwapa elimu Wananchi kuwa CCM sio ile ya enzi za Mwalimu bali sasa ni ya matapeli na wapigaji.

Haya ndio mapinduzi ya kweli kama ya yale ya Cuba yaliowaondoa wanyonyaji

..Chadema ina mfumo wa uongozi wa kanda.

..kwa hiyo Mwenyekiti wa taifa, na Katibu Mkuu, hawana mamlaka makubwa ya kuamua yanayofanyika ktk kanda.

..Wanachadema wakijiimarisha ktk kanda zao, Mwenyekiti wa taifa, na Katibu Mkuu, watalazimika kufuata kinachoamuliwa ktk kanda husika.
 
..sio sahihi kusubiri Chadema watufanyie lila kitu.

..wananchi wenyewe tunaweza kuhamasishana kupigia kura chama tofauti na Ccm.
Huwezi kufanya siasa nje ya chama cha siasa. Kama wananchi wanaweza kuhamasishana nje ya Chadema maana yake hakuna haja pia ya kuwa CCM pia
 
..basi wajiunge na chama chochote na wahamasishe ndani ya chama mambo wanayoyataka.
 
..Chadema ina mfumo wa uongozi wa kanda.

..kwa hiyo Mwenyekiti wa taifa, na Katibu Mkuu, hawana mamlaka makubwa ya kuamua yanayofanyika ktk kanda.

..Wanachadema wakijiimarisha ktk kanda zao, Mwenyekiti wa taifa, na Katibu Mkuu, watalazimika kufuata kinachoamuliwa ktk kanda husika.
Kinadharia, ni kama nimekuelewa kuhusu hayo mambo ya kanda, lakini kiuhalisia sijui kama muundo huo umeimarika kiasi cha kuwa na uwezo huo ulio uelezea hapa.

Muundo huo ungekuwa umeimarika vyema, CCM wangelia sana.
 
..basi wajiunge na chama chochote na wahamasishe ndani ya chama mambo wanayoyataka.
Kwani ni lazima niwe ndani ya CHADEMA, au chama kingine kuwakataa CCM na mambo wanayo yafanya?
Kuhamasisha wengine hailazimu kuweka jukwaa na kuita watu waje wanisikilize. Kila mtu asiye kubali mambo ya CCM akiweza kuhamasisha hata jamaa zake tu nyumbani inatosha kabisa kuwafurumusha CCM.

Lakini yote hayo, hayaondoi umuhimu wa CHADEMA au chama kingine chochote kuwa mstari wa mbele kuongoza uhamasishaji huo.
 
Kinadharia, ni kama nimekuelewa kuhusu hayo mambo ya kanda, lakini kiuhalisia sijui kama muundo huo umeimarika kiasi cha kuwa na uwezo huo ulio uelezea hapa.

Muundo huo ungekuwa umeimarika vyema, CCM wangelia sana.

..tuhamasishane kujiunga na vyama mbadala na kuviimarisha tukiwa ndani.
 
Kwanza kabisa ni kuwag'oa viongozi wenye vinasaba na CCM kama Mbowe na Mnyika.

Pili ni kuleta mabadiliko makubwa kwa kuwapa elimu Wananchi kuwa CCM sio ile ya enzi za Mwalimu bali sasa ni ya wapigaji.

Haya ndio mapinduzi ya kweli kama ya yale ya Cuba yaliowaondoa wanyonyaji
Naunga mkono hoja, wamefunga mengi mazuri ila huu wakati wakae pembeni, tubalishe style ya uongozi
 
Kwanza kabisa ni kuwag'oa viongozi wenye vinasaba na CCM kama Mbowe na Mnyika.

Pili ni kuleta mabadiliko makubwa kwa kuwapa elimu Wananchi kuwa CCM sio ile ya enzi za Mwalimu bali sasa ni ya wapigaji.

Haya ndio mapinduzi ya kweli kama ya yale ya Cuba yaliowaondoa wanyonyaji
Huku ccm kuna wanamapinduzi wanafanya kazi hiyo wenyewe. Hawawezi kuiruhusu chadema maana sio chama cha kimapinduzi bali kinatumika na mabeberu kutaka wao kusimika vibaraka wa magharibi kuongoza taifa. Wanamapinduzi ndani ya chama cha mapinduzi wanapambana kila siku na hawatolala kuhakikisha chama chao kinaongozwa na wazalendo wenye kulinda maslahi ya umma wa watanzania.
 
CHADEMA kwa sasa ni mithili ya mwanaume mwenye upungufu wa nguvu za kiume na hayupo tayari kutumia dawa.
 
Kwanza kabisa ni kuwag'oa viongozi wenye vinasaba na CCM kama Mbowe na Mnyika.

Pili ni kuleta mabadiliko makubwa kwa kuwapa elimu Wananchi kuwa CCM sio ile ya enzi za Mwalimu bali sasa ni ya wapigaji.

Haya ndio mapinduzi ya kweli kama ya yale ya Cuba yaliowaondoa wanyonyaji
Mbona ccm ilishakufa mzee sasa hivi chadema wanapambana na serikali,wanasubiri tu serikali iwape ridhaa kushika nchi kidiplomasia
 
Back
Top Bottom