Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 126,600
- 241,428
Wakati wakitangaza wiki ya Maandamano, viongozi wa Chadema walisema kwenye Azimio la Mtwara limeagiza Wanachadema wote walio nje ya Nchi waandae maandamano ya kupinga Ugumu wa Maisha nchini Tanzania na Sheria mbovu za uchaguzi hukohuko walipo.
Ambapo ilielekezwa Maandamano hayo yaishie kwenye Balozi au kwenye Taasisi za Kimataifa, ili kufikisha Ujumbe na kuweka shinikizo la Kimataifa.
Sasa Taarifa tuliyonayo ni kwamba, maandalizi ya jambo hilo yamekamilika katika Majiji kadhaa ya Ulaya na USA, na muda wowote kuanzia sasa Maandamano hayo yatavurumishwa bila huruma yoyote.
Tunawashukuru sana Wazungu kwa kuruhusu Maandamano ya watanzania kwenye Nchi zao huku wakiahidi Ulinzi wa Polisi uliotukuka.