Cha ndimu

umenikumbusha mbali sana.mimi nilikuwa mmoja wapo wa kusuka mpira na kuwauzia madogo nwisho wa siku waliniibia vifaa vyangu ikawa mwisho wa game.sinema yangu imeishia hapo.


swissme
 
kama hiyo ardhi ilivyo ukitoka hapo umepaukaa kuoga hutaki lkn kula unataka,kama ni ubweche unawahi kurudi na kuoga mapema..sembo imenikuza
dah you remind me those day
 
enzi kuna timu mtaani inaitwa chelsea, tandale shule hiyo, mzee mzima nilikuwa nakamatia namba11, kama napiga vile nawavuta wawili watatu nampa mwanangu saidi kiduarisho anaweka kambani.. utoto raha
 
Mwenye mpira lazma apangwe! La sivyo hakuna kucheza


Nimependa hii...Mara nyingi wenye mpira walikuwa hawajui kucheza, akichezewa rough (rafu) ndogo tu anaweka mpira kwapani kutaka kuondoka, halafu inabidi mmbembeleze weee, mpaka anakubali.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…