Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,616
- 1,196
CDE. SILAF JUMBE MAUFI, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa ameanza ziara rasmi akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Rukwa itakayohusisha Mikutano ya ndani na Mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 02 - 06 Juni, 2025.
Ziara inalenga kukutana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata, Mabalozi, Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji, Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji wa Jumuiya Ngazi ya Kata, Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya wa Matawi.
Ziara hiyo itakuwa na Mikutano ya ndani (Kujenga, Kuimarisha Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake) na Mikutano ya hadhara (Kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi) ambayo inatarajia kuanzia Sumbawanga Mjini