CDE. Deborah Tluway ashiriki Program of Shaping the Shared Future in Beijing, China 🇨🇳

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,687
1,238
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kutoka Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa, Komredi DEBORA JOSEPH TLUWAY ni miongoni mwa viongozi vijana wa UVCCM wanaoshiriki Mafunzo kwaajili ya viongozi vijana yanayohusisha Vyama vya Ukombozi Barani Afrika ikiwemo SWAPO na ZANU PF yanayofanyika Beijing, China.

Debora Joseph Tluway ni miongoni mwa viongozi wa UVCCM wanaoshiriki Mafunzo hayo yaliyo chini ya Program of Shaping the Shared Future na yanahusisha vijana mbalimbali kutoka nchi nyingi za Bara la Afrika

"Nina furaha kusema kwamba Tanzania ni nchi yenye Amani, Upendo na Umoja (Mshikamano) ikiwa na fursa nyingi sana katika Utalii, Kilimo, Madini (Tanzanite), Uvuvi na fursa mbalimbali Nawakaribisha sana Tanzania" - Ndugu Debora Joseph Tluway, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa

"Tanzania ni nchi nzuri inayoongozwa na Kiongozi Makini, Imara, Jasiri na Shupavu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" - Ndugu Debora Joseph Tluway

"Napenda kuuambia Ulimwengu kuwa CCM na Jumuiya zake itaendelea kushirikiana na CPC (China) na Vyama vingine vya Ukombozi Barani Afrika (For the sake of our mutual friendship and benefits)" - Ndugu Debora Joseph Tluway

"Mtakubaliana na mimi kuwa urafiki na ushirikiano wa Vyama vya CCM na CPC pamoja na Serikali ulijengwa katika Msingi Imara (Solid Foundation) ulioanzishwa na waanzilishi wa mataifa yetu mawili yaani Mwenyekiti Mao Zedong (China) na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanzania) ambapo China iliamua kuisadia Tanzania kuleta Ukombozi (Redemption of Southern African Countries) wa FRELIMO (Mozambique), ANC (South Africa), SWAPO (Namibia), ZANU PF (Zambabwe) & MPLA (Angola)" - Ndugu Debora Joseph Tluway

"Tanzania iliweza kuendesha harakati za kuitaka nchi ya Marekani (USA) kuitambua nchi ya China kama Mjumbe wa Kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ujenzi wa Reli ya Tanzania - Zambia (TAZARA) ni ishara ya ushirikiano mzuri kati ya China na Tanzania" - Ndugu Debora Joseph Tluway

"Miaka 45 ya Ushirikiano wa Vyama vyetu vya Siasa tumekuwa tukisaidiana kila mmoja katika mambo mbalimbali. Katika miaka ya hivi karibuni tumeona alama ya ushirikiano wetu kwa uanzishwaji wa Mwalimu Julius Nyerere Leadership School kilichoundwa na Vyama Sita vya Ukombozi Barani Afrika kilichopo Kibaha, Tanzania" - Ndugu Debora Joseph Tluway

WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.17.30.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.18.52.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.18.54(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.19.58.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.19.58(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.19.59.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.19.59(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.20.00.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.20.00(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.20.01.jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.20.01(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-06-06 at 16.20.02.jpeg
 
..vijana acheni upumbavu.

..Uvccm sio makomredi.

..mkiwa makomredi wakina Kingunge Ngombale Mwiru, Gisler Mapunda, Sheri Taki, Daudi Mwakawago, watakuwa nani?
 
Back
Top Bottom