Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 2,205
- 3,790
Asalaam Aleykum wana jamvi.
Taarifa zilizogonga vichwa vya habari wiki hii ni kung'olewa madarakani kwa chama tawala cha Botswana ambacho kimekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50.
Hizi habari si njema sana kwa vyama vilivyoleta uhuru na ambavyo bado viko madarakani, ikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wanasema mwenzio akinyolewa, zako tia maji.
Hivyo CCM wanayo kazi ya kufanya kama kweli bado wanayo nia ya dhati ya kuendelea kubaki madarakani. Upepo wa sasa wa kisiasa duniani na Afrila kwa ujumla, si mzuri kabisa hasa kutokana na mambo ya kiuchumi yalivyo na maisha yamekuwa magumu sana kwa watu wa hali ya chini ambao ndio wengi.
Hayati Mwl. Julius K. Nyerere aliwahi kuwaasa CCM na vyama vingine vya siasa kwamba, wanapokwenda kwenye uchaguzi, basi waangalie sana mtu anayekubalika kwa walio wengi.
Hivyo CCM kutokana na umakini wake na uzoefu wao, nawashauri 2025 wafanye "surprise" kama ile ya 2015. Watuletee "jembe" kweli kweli.
Kama mtayapuuza haya ninayowaasa, basi matokeo ya uchaguzi 2025, yanaweza kuwashangza!
Epukeni kabisa kutuletea mtu/watu ambao hata wakishindanishwa na "mawe", basi watu watakuwa tayari kuchagua "mawe" kuliko aina ya watu mliowaletea.
Katika visiwa vya Ukerewe, kuna kipindi nakumbuka mgombea wa upinzani (Mr. Mataa) tena ambaye hakuwa na elimu kubwa wala utajiri, aliweza kumbwaga tena kwa kishindo kikubwa sana Bi. Beijing ambaye alikuwa ameshalifanya jimbo la Ukerewe kama mali yake Binafsi. Kuja kuchunguza, ikaonekana kumbe Mr. Mataa, alikuwa anafanyiwa kampeni na wana CCM wenzake na Bi. Beijing!
Sasa wana CCM, msijifanye kama sauti/kelele zinazopigwa iwe kwenye mitandao au sehemu zingine, hamzisikii. Najua Watanzaniq wengi ni wavumilivu sana, lakini hata uvumilivu huwa inafika muda unakoma.
Ikumbukwe kwamba Watanzania si "waoga" kama ambavyo wengi wanafikiria, isipokuwa tu wana nidhamu ya kupitiliza. Sasa mtu mwenye nidhamu sana, ukimchukulia "poa", akija kubadilika, anakuwa mbaya zaidi ya wale ambao hawana nidhamu ya kupitiliza.
2025, CCM leteni "majembe", msilete matajiri au wenye vyeo kwa sababu tu ya kuongwa vitu vidogo vidogo au kuahidiwa vyeo.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CCM,
Amin.