CCM "wamemtangaza" mgombea Urais wao wa 2020. Wapinzani wamejipangaje?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Ni wazi kuwa kwa mujibu wa mabadiliko ya katiba ya CCM ya mwaka 2017, Rais Magufuli atapitishwa bila kupingwa kugombea tena Urais kwa kipindi cha pili ifikapo mwaka 2020.

Hii ni sawa na kusema kuwa CCM imeshamtangaza Magufuli kuwa mgombea wao wa kiti cha uraisi mwaka 2020.

Swali linakuja,
Vipi wapinzani wamejipangaje kwa uchaguzi huo?

Nani haswa atakayeweza kukabiliana na Magufuli ambaye kuna kila dalili kuwa kama kutakuwa uchaguzi kwa mujibu wa sheria na katiba hataweza kuvuka?

Lakini pia wamejiandaaje kuhakikisha vyombo, sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi vinaweka misingi dhabiti kuhakikisha uhuru wa kweli katika uchaguzi huo?

Ikumbukwe Watanzania watahitaji sera na strategies mbadala na istarajiwe ukosoaji na kukashifu madhaifu yatakayoonekana kwa awamu hii pekee ndio itakuwa njia ya ushindi.

TAFAKARI.
 
kwa mwenendo na upepo huu wa sasa na kama utaendelea hivi kwa miezi 12 ijayo, wapinzani wanahitaji ingredients zifuatazo kuingia Magogoni 2020 (kama hakutakuwa na uchaguzi kabla ya hapo that is):

1. NEC mpya na huru
2. candidate - hakuna haja ya kuumiza kichwa kwenye hili...hata jiwe tu litashinda!
 
Tegemea kuiona CHADEMA vipande vipande kwenye hili.....Kamwe MZEE hawezi kukubali pesa zake ziendee BURE ili hali T.B joshua AMEISHA MTABIRIA atakUWA RAIS iwapo tu WASIPO FARAKANA wao kwa wao.......Hapa alikuwa anajaribu kumfikishia ujumbe yeyote atakae jaribu kumzuia asigombee URAIS kwa tiketi ya UKAWA japokuwa hadi kufikia 2020 HAKUTAKUWA NA MDUDU ANAEITWA ukawa atadili nae ipasavyo.....yetu macho LEO hii midomo yao na miacho yao kufurahia MIFARAKANO ndani ya CCM as if wao wapo
salama....ni suala la MUDA tu
TUTEGEMEE MZEE kuitwa pandikizi la CCM.....maana hawa kawii kuwadilikia WATU....leo hii mbaya lakini kesho atalambwa miguu......
 
Mbona upinzani wameshatamka kwamba wagombea ni kati ya Tundu Lissu au Zito Kabwe. Wakishindwa hao basi Kingunge atatia timu
 
Wejipanga kwa mbinu ya KUPINGA KILA KITU KIWE KIBAYA AU KIZURI, NI FULL KUPINGA.
 
Hivyo mbona hamuelewi huo uchaguzi wa 2020 hautakuweko, mbona dalili ziko wazi
 
Awe lowassa, awe lissu hata liwe jiwe uchaguzi ukiwa wa huru na haki tutachagua upinzani. Tunachoomba uchaguzi uwe huru tu!!
 
Mbona upinzani wameshatamka kwamba wagombea ni kati ya Tundu Lissu au Zito Kabwe. Wakishindwa hao basi Kingunge atatia timu

Sina hakika. Embu tueleze wametamka wapi na lini mkuu
 
Hivyo mbona hamuelewi huo uchaguzi wa 2020 hautakuweko, mbona dalili ziko wazi

Angalia usijeitwa mchochezi! kwa kutamka manneno yanayoweza kuchongnisha wananchi na serikali yao!
 
Mkuu, hii ni post ya maana sana.hizi posts zinatakiwa zipostiwe kila Mara kuwakumbusha wapinzani kudai tume huru na kujipanga kuhusu kupambana na uharamia wowote ule Wa kura za wananchi. Wapinzani watakuwa ni wapumbavu sana kama watasubiri matokeo kwanza ndio watuambie wameibiwa kura.

Maana mpk sasa Pombe ana uhakika na kura moja tu....ya bashit
 
Kwa heshima kubwa wana jukwaa hili la siasa nawasalimu ..,

Awali ya yote napenda kusema kwa kifupi kuwa nawasilisha maoni yangu hapo juu kwakua ni haki yangu kikatiba kwa UKAWA..,

Mwisho na watakieni siku njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…