CCM Vs Upinzani Bungeni: Demokrasia kwa Vitendo

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,742
40,874
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya vitu ambavyo vinanitatiza ni kuwa kuna watu wanatumia maneno haya mawili kwa kuyachanganya; demokrasia na upinzani. Kwamba, tunapozungumzia “demokrasia” tunazungumzia “upinzani” na tunaposema “upinzani” tunazungumzia wakati huo huo na kwenye pumzi hiyo hiyo “demokrasia”. Hivyo, mtu akipinga “upinzani” anaweza kuchukuliwa kuwa anapinga “demokrasia” na mtu akiunga mkono “demokrasia” basi anaweza kuonekana anaunga mkono “upinzani”. Matokeo yake, hatujaelewa au hatuko tayari kuelewa tofauti ya msingi iliyopo kati ya maneno na dhana hizi mbili.

Demokrasia – kama neno linavyosema ni utawala wa watu; hii ni maana yake ya moja kwa moja. Hii inatofautisha na aina nyingine za utawala kwa mfano utawala unaotokana na agizo la Kimungu (theocracy) kama ilivyokuwa kwenye enzi za utawala wa Mfalme Daudi, au baadhi ya tawala za Kiislamu leo hii au hata utawala wa Kipapa. Utawala wa Maagizo ya Kimungu unaweka uwezo mkubwa wa juu kabisa wa utawala yaani hakimiya (sovereignty) mikononi mwa Mungu.

Aina nyingine ni utawala wa Kifalme (monarchy) ambapo mamlaka ya mwisho wa utawala iko kwa mfalme au Malkia. Wananchi wanakuwa ni walio chini (subjects) ya Mfalme au Malkia. Sehemu nyingi duniani hazina tena mfalme kamili (absolute monarchy) ukiondoa chache. Tawala nyingi zimebakia na wafalme wa heshima au ambao wanashirikisha madaraka yao na viongozi wa kidemokrasia. Hii ni kweli kama Uingereza na Japan. Wafalme ambao wana madaraka ya mwisho kabisa ni wachache kama Mfalme wa Swaziland.

Zipo aina nyingine nyingi za utawala kama wa Kiimla, wa Kichifu, wa Wasomi wachache, wa Wazee n.k Lakini kwa ajili ya mada yetu hapa niseme tu kuwa tunapozungumzia utawala wa kidemokrasia tunamaanisha utawala wa watu wengi au wa wananchi. Huu unaweza kuwa ni utawala wa moja kwa moja au utawala wa uwakilishi – kwamba wananchi wanachagua watu wao kuwawakilisha. Nchi nyingi zinazoitwa za “kidemokrasia” zina mfumo wa uwakiilishi ambapo wananchi huchagua viongozi wao.

Sasa, shida moja ambayo inaonekana kutuvuruga Watanzania ni kuwa maana hii ya demokrasia inataka kupoteza maana; walioshindwa uchaguzi wanataka wawe kama walioshinda uchaguzi, ajenda iliyokataliwa inataka iwe kama iliyokubaliwa, mapendekezo yaliyopingwa kwenye sanduku la kura yanataka kuwa yaliyoshinda kura. Walioshindwa wanataka wachukuliwe kama walioshinda!

Demokrasia inataka tukubali matokeo ya maamuzi ya wananchi; hata kama ni matokeo mabaya kiasi gani au tusiyoyapenda kwa kiasi gani. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema katika mojawapo ya maandishi yake kuwa katika demokrasia wananchi wana haki ya kuchagua Serikali waitakayo hata kama serikali hiyo ni mbaya kisi gani. Na ndio maana kuna vipindi vya utawala ili kwamba wananchi wapewe nafasi ya kusahihisha makosa ya maamuzi yao ya nyuma.

Baada ya Wamarekani kuwa na utawala wa Republican kwa miaka nane ya George W. Bush; walikuwa tayari kwa mabadiliko. Kuna ambao waliona kuwa Bush alikuwa ameharibu jina la Marekani kiasi kwamba hawakuwa tayari kuona Republican wanatawala tena. Kwa kishindo kikubwa mwaka 2008 wakamchagua Barack Obama na kutengua maamuzi yao ya nyuma. Wenzetu wanaelewa maana ya miaka minne ya uongozi; wanajua maana ya kusahihisha makosa. Na wanaheshimu maamuzi yao hayo.

Siyo wote Wamarekani walimpenda Obama, siyo wote wamekubaliana na sera zake kuhusiana na Mashariki ya Kati, Uhamiaji, Haki za Mashoga, Mazingira n.k. Kuna ambao wanampinga na wamempinga toka mwanzo. Lakini, katika kumpinga huku hawaoni kana kwamba wao wanaompinga ndio wenye haki ya kutawala sasa na kuwa ajenda yao lazima Obama aikubali vinginevyo basi anaminya “demokrasia”.

Ni Demokrasia iliyomuingiza madarakani, ndiyo inamfanya atawale.

Uchaguzi wa mwaka jana uliamua nani aongoze nchi. Watanzania walienda kupiga kura na wakachagua viongozi wao. Bahati mbaya kwa sisi wengine ni kuwa tulitarajia upinzani ungechukua viti vingi Bungeni ili kuleta uwiano wa kiutawala; tulitamani kuona kuwa wabunge wengi wa upinzani wangeweza kutoa hata mwelekezo wa uteuzi wa Waziri Mkuu, Spika na mjadala wa Bunge ungekuwa mzuri zaidi.

Kosa ambalo wapinzani walilifanya mwaka jana, na ambalo hawajakubali kuwa wamelifanya na kulijutia ni kuwa walijivuruga wenyewe. Waliwapa Watanzania sababu ya kuwakataa wakati tayari walishawakubali.

Huko nyuma nimewahi kuandika makala moja juu ya jukumu la upinzani siyo kuisaidia Serikali kutawala au kuipa serikali mawazo mazuri – jukumu la upinzani popote duniani ni kujitahidi kuona serikali iliyoko madarakani inashindwa, inaanguka ili wao waweze kuingia madarakani. Mpinzani anayetaka kuisaidia serikali itawale vizuri anapaswa kujiunga au kuiunga mkono serikali na kutoa mawazo yake huko. Upinzani unaweza kuwa na mawazo mazuri sana, na unaweza kuwa na ajenda nzuri zaidi; lakini ajenda hiyo haipaswi kusimamiwa na watawala; wapinzani wana ajenda yao na mipango yao.

Sasa, kama wapinzani wanataka kuongoza Bunge wanatakiwa kushinda wabunge wengi; period. Wanatakiwa kuwa na wabunge wengi kutoka majimboni ili waweze kuamua Spika na Naibu Spika anakuwa nani. Lakini hata wasipokuwa navyo wanatakiwa kuwashawishi walio wengi (majority) kukubaliana nao. Na walio wengi wanapaswa kusikiliza hoja za walio wachache lakini hawalazimiki kukubali. Maana demokrasia siyo tu kukubali lakini pia kukataa.

UKAWA walifanya makosa mwaka jana; makosa ambayo ni lazima wayamiliki. Waliacha ajenda yao na wakachukua ajenda isiyo yao. Walivuruga uongozi wao kiasi kwamba wakapoteza maana ya kuongoza. Waliamua kufuata. Leo hii, wanaaamini bado wana uhalali wa kusema “tunaongoza”. Uhalali huu hawana, wameupoteza. Wakitaka kuwa nao kwanza kabisa ni lazima wakiri makosa yao yaliyovuruga harakati za upinzani, na wawaombe radhi Watanzania.

Kuendelea kususa Bungeni kwa sababu ya kujaribu kuoneshana ubabe hakuwafanyi wawe sahihi. Hawawezi kulia sasa kama wao wenyewe walikuwa wanachezea kiwembe. Baadhi yetu tumekuwa tukiamini kabisa upinzani ili ushinde ni lazima uwe bora kuliko CCM; siyo uwe sawa na CCM. CCM waliporusha madongo wapinzani walianza kurusha madongo, CCM walipofanya baya hili na upinzani wakataka kufanya baya lile ili nao waonekane wanaweza; matokeo yake Watanzania hawakuona tofauti kubwa ya kiuongozi kati ya CCM na wapinzani.

Hivyo, wananchi Watanzania waliamua kwa njia ya kidemokrasia kuwa Magufuli awe Rais wao. Na Wananchi hao hali waliamua kuwa wabunge wengi watoke CCM. CCM kuendelea kutawala siyo kwa sababu nyingine isipokuwa makosa ya upinzani wenyewe. Kuendelea kuililia CCM ni kutaka kukwepa hoja iliyopo. Upinzani umejivuruga na unaendelea kujivuruga.

Hili si tatizo kwa demokrasia; hili ni matokeo ya demokrasia! Demokrasia haiminywi; wapinzani wamejiminya wenyewe! Haki ya maoni haiku kwa upinzani tu; bali pia kwa watawala; haki ya kupinga haiko kwa wapinzani tu hata kwa watawala. Yote hii ni demokrasia.

Tunapotetea demokrasia tujue kuwa hatutetei demokrasia inayotufaa sisi tu; tunatetea kanuni za msingi za demokrasia.

Wananchi wakiona wamefanya makosa makubwa, wakiona demokrasia haijawaletea mabadiliko waliyoyatarajia, wananchi hao hao kwa kutumia demokrasia wataiondoa serikali hiyo na kuweka nyingine.

Kinachoendelea nchini kati ya upinzani na watawala si kingine bali demokrasia kwa vitendo. Tujifunze kwa Wamarekani nan chi nyingine za kidemokrasia. Kuna aina nyingi za utawala duniani, tumeamua kufuata utawala wa kidemokrasia; tuwe tayari kuishi na matokeo ya aina utawala huo
 
Well said. Kichwa chenye mvi ndio chenye hekima.
 

Shutting up your mouth is also a good democracy
 
Demokrasia kwa vitendo huwa inabadilika kutokana na mazingira mbalimbali. Inabadilika kutokana na watu, mahali, wakati nk. Kwa sasa Tz demokrasia kwa vitendo ni kufunga midomo kwa plaster na karatasi.
 
Demokrasia kwa sasa ni kuwakataza wanaCHADEMA kufanya mapenzi na wanaCCM hapo ndipo ukomo wa Kubenea na yamkini viongozi wa UKAWA waliomtuma unapoishia.
 
Tatizo la Mzee Mwanakijiji ni kuwa mzimu wa uchaguzi wa 2015 bado unakusumbua. Yani kwasababu wapinzania na hasa CHADEMA hawakufata matarajio yako umejivika vazi la kuwa vuvuzela wa serikali hii ya tano. Ukweli ni kuwa, kuna mambo mazuri yanafanywa na serikali hii, ila kuna mengi mabaya yanayofanywa pia na ambayo yanatuchefua wananchi wengi. Bandiko lako linasema kuwa demokrasia ni kuchagua na kuweka serikali...unataka kuniambia demokrasia haina mahusiano na kukoselewa, kuonywa, nk? Je, unataka kuniambia, demokrasia haina mahusiano na kuwapa nafasi watu kusema na kuchangia mawazo yao kwenye kuendesha serikali?

Anyway, kwasasa naanza kupata majibu kwanini Mzee Mwanakijiji umepotea kwenye midomo na mawazo wa wanamageuzi wengi. Hakika ikulu ya magogoni na pale Lumumba wamekuajiri rasmi kuwa VUVUZELA. Nakuhakikishia, utapulizwa sana, utatoa sauti sana, ila ushindi ni wa wengine.
 
eti watanzania waliamua kuwachagua wabunge wengi wa ccm. haaa haa uliza kilichotokea huko majimboni. wagombea wengi wa upinzani walichakachuliwa kura zao ili kuhakikisha ccm ina kamilisha idadi ya wabunge wengi kwa kusaidiwa na jeshi letu pendwa la polis. any way naheshimu maoni yako ingawa sikubaliani nayo....
 
Siku hizi Kiwango cha uboho kimeshuka sana pengine ni kwa uzee au msongo wa mawazo, jieleze bakusaidiege ukuu wa wilaya.
 
Ha ha ha ha
Mwanakijiji umewasitukia.

Watu wanafikiri demokrasia ni uhuru wa kuandamana na kupiga siasa majukwaani. Kifupi kabisa ni kwamba.

Democracy is government by the people. Sasa UKAWA mtuambie govement yenu ipi inayominywa na MAGUFULI?

UKAWA mjifunze kutofautisha kati ya haki na demokrasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…