CCM Simiyu Yampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaletea miradi ya maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,617
1,196

CCM SIMIYU YAMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU KUWALETEA MIRADI YA MAENDELEO.

LALAGO; MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Shemsa Mohamed amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika wilaya ya Maswa.

Akizungumza Leo na Wananchi wa Tarafa ya Mwagala wilayani humo katika shule ya sekondari ya Lalago katika mikutano yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika eneo hilo.

Amewaomba Viongozi wote kwa ngazi zote kusimamia miradi hiyo ili iweze kuleta tija kwa wananchi pia amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge kwa kazi nzuri anayoifanya pamoja na timu yake kwa ajili ya kusikiliza kero za Wananchi na hivyo kupunguza malalamiko ya Wananchi.

Aidha amewataka Wananchi kukiunga mkono chama hicho cha CCM katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu ili kiweze kuongoza Dola na kuwatumikia Wananchi kwani Maendeleo yameonekana.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-04-21 at 21.25.09.mp4
    29.6 MB
Back
Top Bottom