Lissu: Tusihangaike na udongo, tuhangaike na mikataba na sheria mbovu za madini zilizotufikisha hapa. Tuangalie tulipojikwaa, tusiangalie tulipoangukia.
CCM: Lissu analinda wezi. Mikataba na sheria za madini hazina shida. Shida ipo kwenye udongo wenye makinikia. Tumeibiwa sana kwenye udongo. Hatukubali.
[HASHTAG]#RipotiYaPili[/HASHTAG]
JPM: Tumelogwa na nani? Watanzania tumeibiwa sana. Naagiza mikataba yote na sheria zote za madini zipitiwe upya.
CCM: Rais wetu mzalendo. Amefanya kazi kubwa sana. Tumuombee.!!
[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Lugha ileile aliyoongea Lissu akaambiwa amehongwa, ndiyo aliyoongea JPM leo akaitwa mzalendo. Akili za CCM kama kifurushi cha jaza ujazwe