Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 25,480
- 18,912
Ndugu zangu Watanzania,
Marekani ipo kama ilivyo leo hii ikiwa na nguvu za aina zote kiuchumi ,kijeshi,kiteknolojia N.k. ni kazi na akili kubwa ya hali ya juu inayotokana na watu walio katika Taasisi hizo bora kabisa za kijasusi na kipelelezi Hapa katika uso wa Dunia ,ambapo moja iliundwa mwaka 1908 ambayo ni FBI na nyingine 1947 ambayo ni CIA. Ambapo Taasisi hizo zenye uwezo mkubwa sana wa kijasusi unaoifanya marekani kuwepo kila mahali na kujuwa kila kinachoendelea katika kila nchi na na chochote kinacho hatarishi usalama wake na maslahi yake popote pale katika Dunia hii. Ni kwa kupitia Taasisi hizo ambapo mwaka 2011 Osama Bin laden alijikuta akinyakuliwa ndani ya nchi ya pakistani karibu kabisa na kambi ya jeshi lenye zana zote za kivita lakini pasipo kuonekana hata katika Rada zake za kijeshi.
Ukiiangalia CCM ya leo chama kiongozi Barani Afrika,Chenye mtandao mpana na imara wa kiuongozi,chenye mizizi mirefu na iliyojikita kila mahali,chenye kuaminika na kuaminiwa na Taasisi mbalimbali utagundua kuwa ni sawa na CIA na FBI ya Marekani. Hakuna chama cha upinzani hapa nchini chenye uwezo wa kuihujumu CCM ,kupanga mipango ovu zidi ya CCM pasipo kujulikana . CCM ya leo ina uwezo wa kujuwa chochote kinachokuwa kinapangwa na kuazimiwa na kamati kuu ya CHADEMA hata kabla wajumbe wake hawajapiga picha ya pamoja au kutoka mlangoni.
CCM Ina uwezo wa kujuwa nani kasema nini ndani ya kamati kuu ya CHADEMA au chama chochote cha upinzani hapa nchini, ina uwezo wa kujuwa nani Kaunga nini ,nani kaanzisha hoja fulani na nani ana msimamo na mawazo gani juu ya jambo fulani au mawazo hatarishi kwa chama na Taifa letu. Kwa ufupi ni kuwa CCM ipo mbele ya vyama vyote vya upinzani hapa nchini, ndio maana wapinzani kabla ya kutoka nje ya ukumbi wa kikao chao mipango yao inakuwa inaeleweka na mikakati yao yote. CCM hii Ina uwezo wa kuwaanzishia Hata ajenda au hoja au mgogoro ndani kwa ndani ya kamati kuu za vyama vya siasa na kuweka mkwamo kwa kutumia vinywa vyao wenyewe pale itakapobidi kwa maslahi ya Taifa letu.
Hii yote ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na CCM kwa miaka mingi sana. Hii ni kutokana na ukweli kuwa CCM na Tanzania Ni kama ngozi na mwili wa mwanadamu ambapo huwezi ukatenganisha au kumchuna mtu ngozi halafu utegemee abakie salama. Ndio maana wenye kuelewa mambo hayo na kuifahamu CCM na mfumo wake tunakuwa tunawashaangaa watu wanaosema kuna watu au mtu fulani alikuwa upinzani na ameingia majuzi tu na kupewa cheo kikubwa ndani ya CCM huku vijana wapambanaji wa muda wote wakiwa wapo. na kuwatukana kuwa ni machawa au madodoki wanaotumika hovyo na huku wapinzani wakija kukaa juu yetu.
Mimi binafsi huwa nacheka sana na kuwaona kuwa ni wachanga katika siasa zetu na bado hawajailewa vizuri CCM .Maana wangekuwa na akili wangejiuliza ilikuwaje mh lowasa ambaye hata gwanda za chadema alikuwa hapendi kuzivaa alikuja ndani ya wiki moja na kupewa nafasi ya kugombea? Kwanini alikuja CHADEMA chama kilichokuwa kinamwita fisadi kwa miaka nane mfululizo? Je chadema ile yenye ushawishi mmewahi kuiona tena mtaani kwenu? Nguvu ile ipo tena? CHADEMA inaweza kuitisha maandamano yakafanyika kwa sasa? Mnakumbuka mh lowasa alikuwa na viongozi gani wastaafu alioambatana nao? Aliwaambia nini? Kwa ufupi ni kuwa hapa nchini hatuna upinzani na wala hatujikuwa na upinzani.sisi sote ni Wana CCM japo mwingine anaweza akaanzia huku na mwingine huku ila mwisho wa siku Bendera yetu ya Taifa na jina la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ndio Dini yetu,kabila letu,Salamu yetu,pumzi yetu,Damu yetu na mboni yetu.
Usipoyajuwa haya utahangaika sana,utateseka sana,utaumia,kulia machozi ya Damu ,kutukana na kubeza sana lakini ukija kujuwa ni upo mwishoni sanaaa mwa kila kitu na huna uwezo wa kufanya chochote kile. CCM Ndio Tanzania yenyewe na Tanzania ndio CCM yenyewe.Tutailinda kwa jasho ,Damu na machozi Bendera yetu ya Taifa .Hilo kila mtanzania analitambua na ndio maana hata uitishe maandamano leo hii hayupo wa kukufuata wala kuunga mkono azima yako hiyo chafu.
Vijana wapambanaji ambao mnaipenda CCM na Taifa letu msitishwe wala kukatishwa Tamaa na maneno ya wapinzani kuwa ninyi mnatumika huku vyeo vikibebwa na wageni. Jibu ni kuwa hayupo mgeni ndani ya CCM wala wakuja wala mwenye kamba mguuni.sisi sote ni wamoja na kila mmoja wetu anatekeleza majukumu yake kulingana na mahali alipo kwa adhima ya kutetea chama chetu na taifa letu. Taarifa ni ushindi na ni nguvu katika vita vya aina yoyote ile. Na ili CCM Chama chetu hiki kiwe na Taarifa kutoka kila chama au eneo au Taasisi kinapaswa kuwa na watu watakaoanzia huko au kupitia huko kwa maumivu,vipigo,jasho,machozi ya Damu,kufukuzwa kazi,kufungwa ,kupigwa mabomu ya machozi ili tu waweze kuaminiwa na kuwa mezani pao na katikati yao kwa masilahi mapana ya chama na Taifa letu. Maana kuna taarifa kuzipata yahitaji jasho,maumivu machozi uyapitie tu. CCM yetu imepitia hayo yote ndio maana Inaendelea kuwa chama kiongozi barani Afrika na Imara sana kila uchwao.
Chapeni kazi vijana wenzangu katika kukitetea chama chetu na Taifa letu ,msirudi nyuma wala kurudishwa nyuma. Wapo tulio nao ndani ya chama lakini pia wapo wenzetu wazalendo wa dhati wapo upande wa pili na wakati mwingine tunawapitisha kwenye bonde la uvuli wa maumivu na jasho ili wapate kuwa kama wao. Maana huwezi ukavaa suti katika mchezo wa mpira,huwezi kusimamisha shingo mahali panapokuhitaji kuinamisha shingo. Tusonge mbele kwa kishindo wana CCM wenzangu, Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.