CCM ni chanzo cha mafuriko yanayozikumba kaya zetu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,428
13,936
Tumetawaliwa na chama kimoja (CCM) tangu nchi ipate uhuru. Serikali ya CCM inahusika na makazi holela yanayokumbwa na mafuriko tunayoyashuhidia yanayosababisha maafa na hasara kubwa wa raia na kodi zetu.

Seikali imeruhusu watu kujenga na kulima popote bila kujali kuna hatari gani. Serikali haina majibu ya raia wanaokata misitu kwaajili ya kuchoma mkaa, kupata kuni za kupikia na miti ya kujengea nyumba zao. Hata mawaziri tunatumia mkaa kupikia kwenye majumba yao.

Huwa najiuliza ni sababu zipi serikali hii imeruhusu watu kujenga mabondeni, kando ya mito na kwenye kuta za milima bila kukatazwa? Ni sababu zipi hata tanesco, dawasa na serikali kupeleka huduma mabondeni na kando ya milima?

Haina watalaam wa mipango miji?
Ni silaha ya kupata kura? au
Ni sababu za rushwa?
 
Acha Ukuda 🐼
Unaruhusu watu wajenge mabondeni, wakikumbwa na mafuriko unapanda helikopta kwenda kuwahani na kuwaahidi misaada ya viwanja sehemu nzuri iyokuwa na mafuriko. Akili za aina hii ni kwa raia malofa tu. Ina maana CCM haikujua mapema kuwa kuna sehemu kuna viwanja vizuri hadi wakumbwe kwanza na mafuriko?

Mjumbe wa nyumba kumi, serikali ya mtaa/kitongoji/kijiji, mtendaji kata, diwani, mbunge, katibu tarafa, Mkuu wa wilaya na mkoa wooote hao hawakujua kuwa wananchi wanajenga sehemu hatarishi. Ni upuuzi tu. wananchi mazuzu wanashangilia serikali inapowapelekea magodoro ya mafuriko ya bonde la msimbazi, rufiji, hanang, nk.
 
Siyo kila kitu ni cha kulaumu Serikali au CCM kama ulivyodai, binafsi nilisikiliza Mahojiano ya Mtangazaji wa Clouds TV na baadhi ya Watu wa maeneo ya Rufiji ambapo kuna Mafuriko, Watu hao wamekiri kuwa Serikali iliwataka wahame maeneo hayo hatarishi siku nyingi za nyuma.

Sambamba na hilo walishapewa hadi viwanja ili wahamie huko, lakini Watu hao licha ya kupewa viwanja eneo lingine ili wahame eneo hilo hatarishi lakini bado wameendelea kurudi maeneo hayo baada ya Mafuriko kuisha.

Ulitaka waondolewe kwa nguvu ili uje una hoja nyingine? Au ulitaka nini kifanyike zaidi ya Elimu iliyotolewa na kupewa viwanja?
 
Umewaza vizuri.

Kodi ya pango wanachukua, hati wanatoa mabondeni, lakini yakitokea mafuriko, hawahusiki!!
 
Tumetawaliwa na chama kimoja (CCM) tangu nchi ipate uhuru. Serikali ya CCM inahusika na makazi holela yanayokumbwa na mafuriko tunayoyashuhidia yanayosababisha maafa na hasara kubwa wa raia na kodi zetu.

Seikali imeruhusu watu kujenga na kulima popote bila kujali kuna hatari gani. Serikali haina majibu ya raia wanaokata misitu kwaajili ya kuchoma mkaa, kupata kuni za kupikia na miti ya kujengea nyumba zao. Hata mawaziri tunatumia mkaa kupikia kwenye majumba yao.

Huwa najiuliza ni sababu zipi serikali hii imeruhusu watu kujenga mabondeni, kando ya mito na kwenye kuta za milima bila kukatazwa? Ni sababu zipi hata tanesco, dawasa na serikali kupeleka huduma mabondeni na kando ya milima?

Haina watalaam wa mipango miji?
Ni silaha ya kupata kura? au
Ni sababu za rushwa?
Kuna kifo cha taaluma ya Mipangomiji ktk nchi hii, na hata ktk nchi zingine karibia zote za ki-Afrika.
Makazi holela na duni Ndio imekuwa ishara ya maisha ya watu Weusi hapa duniani
 
Siyo kila kitu ni cha kulaumu Serikali au CCM kama ulivyodai, binafsi nilisikiliza Mahojiano ya Mtangazaji wa Clouds TV na baadhi ya Watu wa maeneo ya Rufiji ambapo kuna Mafuriko, Watu hao wamekiri kuwa Serikali iliwataka wahame maeneo hayo hatarishi siku nyingi za nyuma.

Sambamba na hilo walishapewa hadi viwanja ili wahamie huko, lakini Watu hao licha ya kupewa viwanja eneo lingine ili wahame eneo hilo hatarishi lakini bado wameendelea kurudi maeneo hayo baada ya Mafuriko kuisha.

Ulitaka waondolewe kwa nguvu ili uje una hoja nyingine? Au ulitaka nini kifanyike zaidi ya Elimu iliyotolewa na kupewa viwanja?
Sio kweli, kama sehemu ni hatarishi kwa mlipa Kodi na hata kwa watoto serikali lazima inapaswa kuzuia kwa nguvu isijengwe. Nyumba hizo za mabondeni simesambaziwa huduma za umeme, maji, barabara, shule, zahanati na wenye nyumba wanalipia Kodi majengo Yao hayo.

Serikali inashindwa kuwaondoa kuogopa kukosa kura? Watendaji wa serikali kula rushwa au uzembe?

Baada ya watu kusombwa na maji serikali inatumia Kodi zetu kuhudumia watu waliojenga mabondeni.
 
Eti Chama na serikali nao wanashangaa nyumba na mashamba ya bondeni yamesombwa na maji kama vile walikuwa hawajui kuwa Kuna watu wanaishi mabondeni. Wanajenga bondeni tangu tofali la kwanza hadi la mwisho bila kuambiwa na serikali kuwa eneo Hilo halikengwi, acha kujenga, bomoa msingi wako. Wenye vyeti vya mipingo miji hawana ajira..
 
Sio kweli, kama sehemu ni hatarishi kwa mlipa Kodi na hata kwa watoto serikali lazima inapaswa kuzuia kwa nguvu isijengwe. Nyumba hizo za mabondeni simesambaziwa huduma za umeme, maji, barabara, shule, zahanati na wenye nyumba wanalipia Kodi majengo Yao hayo.

Serikali inashindwa kuwaondoa kuogopa kukosa kura? Watendaji wa serikali kula rushwa au uzembe?

Baada ya watu kusombwa na maji serikali inatumia Kodi zetu kuhudumia watu waliojenga mabondeni.
Kipi ambacho siyo kweli kwenye maelezo yangu? Unachotakiwa kuelewa si maeneo yote hatarishi yalikuwa hivyo tangu awali, Kuna baadhi ya maeneo yalikuwa salama lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira maeneo hubadilika na kuwa hatarishi..

Pale Hanang'i Wananchi wameishi enzi na enzi pasipo majanga yoyote kutokea, eneo kama hilo ulitaka Serikali isipeleke huduma kwa Wananchi wake?
 
Kazi ya serikali ni kulinda raia na mali zao na kutoa huduma kwa kutumia kodi zao. Kumuacha mtu ajenge na kuishi bondeni ni kimlinda raia?
Hivi huyo Raia anayejenga bondeni haoni kuwa ni bonde? Mara ngapi Serikali inawataka Wananchi wahame maeneo hayo hatarishi lakini bado Watu wanarudi? Wengine wamepewa hadi viwanja maeneo salama lakini bado hawaendi huko.

Elimu inatolewa na Mamlaka ya hali ya hewa mara kwa mara hutoa taarifa kuhusu hali itakavyokuwa kwa msimu husika na kutoa ushauri, hiyo nguvu unayotaka itumike ni ipi zaidi ya kutoa ushauri na Elimu kwa Watu?
 
umepewa akili uzitumie wewe pia unakiwango chako cha kujilinda.unapoenda kujenga bondeni serikali ikiwazuia mtasema bonde limeuzwa kwa waarabu.

kalale kwenye reli ikukate miguu alafu ita waandishi wa habari ulaumu serikali kwa kushindwa kufunga breki za treni!.
 
Kipi ambacho siyo kweli kwenye maelezo yangu? Unachotakiwa kuelewa si maeneo yote hatarishi yalikuwa hivyo tangu awali, Kuna baadhi ya maeneo yalikuwa salama lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira maeneo hubadilika na kuwa hatarishi..

Pale Hanang'i Wananchi wameishi enzi na enzi pasipo majanga yoyote kutokea, eneo kama hilo ulitaka Serikali isipeleke huduma kwa Wananchi wake?
Bonde la msimbazi, pale jangwani, na rufiji hapakuwa hatarishi lini? Unawaachia wajenge, unawapelekea umeme, maji, shule zahanati na Kodi ya majengo, siku wakikumbwa na mafuriko serikali inawapa viwanja bure sehemu salama, chakula, malazi, mavazi na fedha za fidia kuondoka mabondenii.
 
Mkivunjiwa kama alivyokuwa anafanya JPM bado mtalalamika.. kuna mambo mengine ni raia wenyewe na upuuzi wao. Serikali kuna muda inapotezea baadhi ya mambo ili kutoleta sintofahamu kwenye jamii. Nature itawang'oa wote wa mabondeni.
Kama ni upuuzi wa raia kwanini serikali inatumia Kodi zetu kuwapa viwanga na kujengea wapuuzi nyumba sehemu salama baada ya mafuriko? Kwanini wapuuzi wapewe chakula na magodoro ya bure, kwanini wapuuzi walipwe kifuta machozi kwa Kodi zetu.

Mzee makamba alipokuwa mkuu wa mkoa DSM alitaka kuwaondoa watu wa mabondeni kwa nguvu lakini akaambiwa acha tutakosa kura. Shida sio kuwaondoa kwa nguvu Bali ulikuwa wapi wakati wanajenga mabondeni na kupelekewa huduma za umeme na maji?

CCM inatutia hasara kubwa sana. Inatengeneza tatizo na kupongezana wakati wa kulitatua.
 
Tumetawaliwa na chama kimoja (CCM) tangu nchi ipate uhuru. Serikali ya CCM inahusika na makazi holela yanayokumbwa na mafuriko tunayoyashuhidia yanayosababisha maafa na hasara kubwa wa raia na kodi zetu.

Seikali imeruhusu watu kujenga na kulima popote bila kujali kuna hatari gani. Serikali haina majibu ya raia wanaokata misitu kwaajili ya kuchoma mkaa, kupata kuni za kupikia na miti ya kujengea nyumba zao. Hata mawaziri tunatumia mkaa kupikia kwenye majumba yao.

Huwa najiuliza ni sababu zipi serikali hii imeruhusu watu kujenga mabondeni, kando ya mito na kwenye kuta za milima bila kukatazwa? Ni sababu zipi hata tanesco, dawasa na serikali kupeleka huduma mabondeni na kando ya milima?

Haina watalaam wa mipango miji?
Ni silaha ya kupata kura? au
Ni sababu za rushwa?
Kabisa
 
Hivi huyo Raia anayejenga bondeni haoni kuwa ni bonde? Mara ngapi Serikali inawataka Wananchi wahame maeneo hayo hatarishi lakini bado Watu wanarudi? Wengine wamepewa hadi viwanja maeneo salama lakini bado hawaendi huko.

Elimu inatolewa na Mamlaka ya hali ya hewa mara kwa mara hutoa taarifa kuhusu hali itakavyokuwa kwa msimu husika na kutoa ushauri, hiyo nguvu unayotaka itumike ni ipi zaidi ya kutoa ushauri na Elimu kwa Watu?
Raia wengi hawana akili hizo unazofikiria wewe, ndio maana kuna idara za mipango miji na watumishi wanaolipwa huko.
 
Siyo kila kitu ni cha kulaumu Serikali au CCM kama ulivyodai, binafsi nilisikiliza Mahojiano ya Mtangazaji wa Clouds TV na baadhi ya Watu wa maeneo ya Rufiji ambapo kuna Mafuriko, Watu hao wamekiri kuwa Serikali iliwataka wahame maeneo hayo hatarishi siku nyingi za nyuma.

Sambamba na hilo walishapewa hadi viwanja ili wahamie huko, lakini Watu hao licha ya kupewa viwanja eneo lingine ili wahame eneo hilo hatarishi lakini bado wameendelea kurudi maeneo hayo baada ya Mafuriko kuisha.

Ulitaka waondolewe kwa nguvu ili uje una hoja nyingine? Au ulitaka nini kifanyike zaidi ya Elimu iliyotolewa na kupewa viwanja?
Usitetee uzembe wa serikali. Uhusiano wa serikali na raia ni kama uhusiano wa baba na mwana, na kwa muktadha wa hoja inayojadiliwa, uhusiano huu ni kama wa mzazi na mtoto mdogo ambaye akili haijakomaa. Unamkataza mtoto asitende jambo fulani ni hatari, lakini bado anarudia. Hapo lazima utumie nguvu kwa manufaa ya mtoto. Utetezi kwamba waliambiwa waondoke au waliondoshwa na kulipwa fidia kisha wakarudi ni wa ovyo kabisa. Serikali Ina kila kitu- mamlaka, utaalamu, uwezo wa fedha kutekeleza jambo, rasilimali watu nk.
Ni kama vile unakuta mji unaanza mahali, mji unakua kidogo kidogo mpaka unakuwa mji mkubwa. Pale serikali inakusanya kodi kwa wakazi wa eneo lile, watu wakiomba wanaunganishiwa umeme, maji etc. Lakini utakuta mji huo hauna huduma kama shule ya msingi/sekondari, hakuna eno la soko, hakuna zahanati/kituo cha afya, eneo la kuzikia nk. Ni wajibu wa serikali, kwanza kutoa idhini kwamba eneo husika linafaa kwa makazi, na iweze kupangilia mji kwa kutenga maeneo kwaajili ya huduma mbalimbali.
 
Back
Top Bottom