The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,930
- 2,909
Kwa namna ccm inavyoendesha siasa zake binafsi ndani ya chama, yaani mnampa fomu mgombea mmoja. Ukiangalia kwa makini kilichojificha nyuma ya kituko hicho ni kuogopa changamoto za ushindani ndani ya chama ingawa changamoto hizo zingesaidia sana wananchi kupata chaguo bora la wakati ila wao wameweka mazingira ya kuogopa minyukano ya kisiasa.
Ulemavu huo huo wameuleta kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji, ambapo eti waziri kada wa ccm mjumbe wa ccm na waziri wa ccm asimamie zoezi za uchaguzi ambao chama chake pia ni washindani.
Sijawahi kusikia wala kuona kwa mataifa yaliyo serious na demokrasia eti kuna upuuuzi wa namna hii.
Naomba nikiri kuwa mimi si miongoni mwa watu wanaoamini kwamba wapinzani wangefanya makubwa sana kwenye uchaguzi huu hata kama wangeachiwa goli wapewe na penalty ila natamani ccm ingeacha game ichezwe fairly.
Ccm kabla ya kujisifu kwamba ni kubwa itanue mbawa za demokrasia na sio kuja na mapambio mengi yanachosha.