Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,366
3,787
Wakuu,

CCM hivi hamuoni vibaya? Mpaka sasa Club House haipatikani halafu tena hao kunyanyua midomo eti mnataka kufungua X(Twitter) kwa kisingizio eti inahamasisha maudhui ya Ushoga!


Huu ni mtandao pekee ambako kuna maudhui ya ngono nchini? Kuna Instagram, Tiktok, Facebook, huku hakuna maudhui ya ngono? Channeli za nje kwenye TV hazina maudhui ya ngono? Nchi ambazo tuna mashirikiano nayo hakuna ambazo wana mpaka sheria za kulinda wanaojihusisha na ushoga na karibu zote kujihusisha na tasnia ya filamu za maudhui ya ngono?

Basi Tanzania IKATE mawasiliano na Dunia, tujitenge na wote wanaambao kwa namna moja au nyingine wanaruhusu maudhui haya kuendelea. Yaani mna act utafikiri maudhui haya yameanza kufanywa leo.

Watu tunatumia mitandao kwa matumizi mbalimbali, unajua mtoto wako harusiwi kuangalia maudhui ya aina fulani msimamie mtoto wako asiangalie. Tanzania kuna uchafu unaendelea hata nchi zilizoruhusu mauzui hayo zikasome. Afu mnakuja na sababu zenu za kipumbvu hapa, shame on you!

Kwanza kama wananchi tuliopewa tuliyohakikishiwa haki hii ya kujieleza/kuwasiliana na kutafuta na kutoa taarifa TUNADEMAND Club House ifunguliwe, sababu mnaminya haki yetu ya kikataba, na kama mmefikiria hata kwa dk moja kuzuia mtandao huu wa X(Twitter) TUNADEMAND muachane na mpango huo mara moja.

ccm xxx.jpg
ccm xx.jpg
ccm xxxx.jpg
ccm xxxxx.jpg

Na mlivyokuwa wajinga sasa, mnaenda kufungua vi account vyenu uchwara na kuvisha rangi za vyama vingine eti tuone manungwa mkono na watu wengi! Mbinu zenu zile zile za kipumbavu. Wakati huu tunasema hapana. Tanzania siyo SHAMBA la BIBI enu kwamba mna uwezo wa kuifanya mtakacho na wote tuake kimya. Yaani kadri siku zinavyoenda manzidi kututia aibu na kutuonesha serikalini kumejaa vichwa maji.

Ona huyu mjinga naye, unauza utu wako na future ya vizazi vijazo kwa pesa ambazo mwisho wa siku unaenda kuzaicha chooni. Wazazi wa hivi mnafanya hata watoto wenu waishi kwa tabu. Mtoto hawezi kujivunia kuwa na mazi wa aina hii anayefikiria tumbo lake muda wote utafikiri yupo peke yake Duniani!

Tuna mfumo wa Demokrasia, tuonyesheni ukomavu kwenu kwenye siasa safi, mshinde kwa hoja na uwezo wenu, na sio ubabe wenu wa kipuunzi wakati utendaji ni 0.

Bure kabisa nyie!

====

Pia soma:
 

Attachments

  • ccm xxx.jpg
    ccm xxx.jpg
    104.4 KB · Views: 7
Tumewashtukia! Wanafanya maandalizi ili kipindi cha uchaguzi kikifika wazime mitandao! Ndio zao hawa,wana hila sana hawa! Bure kabisa
 
Back
Top Bottom