CCM kuubeba msiba wa Lowassa bila kumuomba kwanza msamaha kwa mliyomtendea ni aibu

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,483
2,386
Watanzania poleni sana kwa kuondokewa na kipenzi cha Watanzania na ambaye ni Rais wa Mioyo ya Watanzania Hayati Edward Lowassa.

Nimekuwa naufutilia Msiba huu toka ulipotokea na kuwaona Viongozi wa CCM wakiwa Mstari wa mbele katika Msiba huu kama vile aliyefariki ni Kiongozi wao kumbe ni Kiongozi waliyemkataa hadharani na Kumtukana na Kumkejeli sana.

Hayati Edward Lowassa alifanyiwa Mambo 4 na CCM yasiyofaa. Mambo hayo ni;

1. Kumwondoa Uwaziri Mkuu kwa kashfa ya kutunga ya Richmond.
2. Kumkata jina lake kwa mizengwe katika kugombania kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu 2015 licha ya kuwa na sifa stahiki.
3. Kumtukana na kumkejeli katika Mikutano ya Kampeni ya CCM kulikofanywa na Viongozi wa CCM
4. Kumwibia kura za Urais alizozipata kama Mgombea Urais wa CHADEMA na kumshinda Mgombea wa CCM kipitia Kituo cha Uibaji kilichokuwa Masaki kipitia Bao la Mkono.

Matukio yote hayo yalifanywa na CCM na hakuna hata siku moja CCM imemwomba Radhi Hayati Lowassa kwa niaba ya Wanachama wake.

Nakipongeza Chama cha CHADEMA pamoja na kumwita Hayati Lowassa Fisadi ilijisafisha kwa kumpokea na kumpa Heshima ya kugombea Urais kwa Bendera yao.

Ushauri kwa CCM wakati wa mazishi tumieni nafasi hiyo Kutubu kabla ya Hayati Lowassa kuzikwa kinyume chake Mzimu wa LOWASSA hauta waacha Hayati LOWASSA kafa na Kinyongo juu ya CCM.
 
CCM ni MABINGWA wa SIASA za FITNA KULOGANA na KUNYWESHANA SUMU pamoja na SINDANO ZA SUMU.
 
Kwahiyo CHADEMA walitubu kwa kumsafisha na LIST of SHAME?
Kwamba ile kashfa haikuwa kweli CHADEMA walitunga UONGO, basi hakuna kitu CHADEMA watastahili kuaminika.
 
Back
Top Bottom