Julai tunafanya safisha safisha ya chama yale masalia ya mtandao get ready
Harafu Chadema mambo ya kuchukua masalia yanayotoka Ccm acheni kabisaaaa.. Mnatupa wakati mgumu kuwatetea humu ndani
kwenye dampo letu pale mtaa wa ufipa kinondoniHayo masalia yanapelekwa wapi mkuu?
Hakuwa na mafuriko huyu?
Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimesema kimeanza kutekeleza mpango maalum wa kuwapatia mbinu wawakilishi wa wananchi wanaotokana na chama hicho ili kubaini wizi ufisadi na ufujaji wa mali za Umma unao fanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali katika miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Mwenekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael Lekule Laizer ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika miji ya Engaruka na Serera na kudai kuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la miradi hewa inayo tokana na watendaji wa serikali kutokuwa waadilifu na uwezo mdogo wa wawakilishi wa wananchi kugundua ufisadi wa mali ya umma.
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Shabani Mdoe amesema kiongozi watakao kiuka maagizo hayo watachukuliwa hatua kwakuwa wakati huu siyo wa kulindana.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli Loata Sanare amewataka wana CCM kuacha mifarakano kwakuwa imekuwa chanzo cha watendaji kutofanyakazi kwakuwa hakuna wananchi wanaowafuatilia utekelezaji wa miradi inayo wahusu.
Chanzo:ITV
Mnaanza na yupi?Nawapa ushauri mafisadi wote ndani ya ccm ,wahamie chadema kabla ya july
Mnaanza na yupi?