CCM kama Wayahudi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,858
Wayahudi walipokuwa wanamsulubisha Yesu walikuwa wanafurahia sana wakidhani wanamkomoa lakini ukweli ni kwamba walikuwa hawajui walitendalo na ndio maana Yesu kabla hajakata Roho pale msalabani alisema: "Baba wasamehe hawa kwakuwa hawajui walitendalo".

CCM nao,kwa waliyoyafanya Dodoma siku mbili zilizopita kwa kuwasulubu wanachama wao huku wakishangilia wakiamini wanawakomoa, hakika ni wazi nao hawajui walitendalo kama ilivyokuwa kwa Wayahudi na bahati mbaya wao hawawezi kusamehewa mbinguni na duniani maana hakuna wa kuwaombea msamaha.

Hawajui walitendalo kwasababu wanayoyafanya yatakuja kuwagharimu huko mbeleni kama tulivyoona mwaka 2015 baada ya Lowassa na makada wengine kuamua kujitoa katika chama hicho na kutimkia upinzani na matokeo yake leo hii kila mtu ni shahidi.

Nina hakika kiongozi yoyote yule wa CCM au mwana-CCM mwingine yoyoye yule leo hii ukimuuliza ni uchaguzi gani ulikuwa tishio kubwa kwao bila kufikiria mara mbili atakujibu ni Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Dodoma kwa sasa naitazama kama Yerusalem mji aliosulubiwa Yesu Kristo ili kuwakomboa wanadamu kwani wanaosubiliwa Dodoma kwa sasa wanasulubiwa ili watanzania wakombolewa.

Dodoma, Jerusalem ya Tanzania.
 
CCCM Ni chama gani tena Mkuu?.

Uongozi wa Kweli siyo Ofisi wala Kitambi,bali ni Karama.Lakini kama wasemavyo ndugu zangu wasukuma kuwa "Masala hulangwa" (Pasco Mayalla utanirekebisha) wakiwa na maana kuwa "Akili hufunzwa",nami ninaongeza kuwa asiyejifunza hafundishiki.

Chama Cha Mafisadi hawajifunzi na kwakuwa hawajifunzi hawatokaa wafundishike.

cc Lizaboni .
 
Mbona hapo nimesharekebisha mkuu!

Back to the topic.Tutasema mengi lakini hawa wenzetu hawana tofauti na Wayahudi waliomsulubisha Yesu maan nao hawajui watendalo.
 
CHADEMA mnapata wapi ujasiri ya kusema vyama vinginge? Zitto, Mwigamba, Kitila Mkumbo mliwafanya nini? Na vipi wale madiwani 5 wa Arusha? Sasa leo mnaona nongwa kwa CCM kusafisha nyumba yao, au walikuwa watu wenu?
Kwa sasa hamuwezi kuelewa mpaka yatimie na nyie endeleeni tu kuigeuza Dodoma kuwa Yerusalem(mji wa kusulubu watu) mtaona matokeo yake ambayo sisi ndio tunayataka.
 
Wasamehe kwani hawajui walitendalo.
Hiyo ni ya Yesu Kristo.
Lakini Nebukadineza yeye ni jino kwa jino.
Kila mwamba ngoma kamba huvutia kwake
 
Ah
 
Mkutano mkuu wa CCM Dodoma umeonekana kuwahusu BAVICHA NA BAWACHA zaidi kuliko CCM,maana ndo wanaoanzisha thread humu za mkutano wa CCM zaidi ya CCM wenyewe.Mpaka wengine wametoa tathmini ya marekebisho ya katiba ya CCM(2017),kana kwamba yanawahusu.
 
Endeleeni kusulubu ili hatimae sisi tukombolewe.
 
Yanayofanywa na ccm yanagusa maslahi ya nchi nzima kwa maana kuwa chama hicho na chama kingine chochote kinashufhulika kitaifa. uwepo wake unagusa watz kwa namna moja au nyingine. kwa muktadha huu lolote linalotokea hapa nchini kila mwenye uchungu na nchi yake ana Uhuru wa kutoa maoni yake juu ya nn hasa kinapaswa kufanyika. huo ndio Uhuru wa kupata na kutoa maoni. hapo haijalishi una chama au hauna. huo ndio uelewa mpana kuhusu Demokrasia
 
Endeleeni kusulubu ili hatimae sisi tukombolewe.
Hao wanaoondolewa CCM ni Team Mamvi(Ulipo Tupo),walikuwa wamesalia tu chamani,sasa wewe upo hapa na story zako za sijui Yerusalemu,hujui madhara yake.Ni wanamtandao wa mamvi,yeye huwa anatengeneza mtandao wake kila anapoenda.Na mshukuru Mungu sasa hivi anasumbuliwa na ugonjwa vinginevyo mngeishakoma ubishi,angehamia huko 2010 CDM ingekuwa tayari na kambi mbili au tatu tofauti.CCM inazidi kujiimarisha,nyie baada ya kumshauri mwenyekiti wenu kujenga hata ofisi,mpo bize humu JF na tathmini za mkutano wa mabadiliko ya katiba ya CCM.Nawauliza tena UNAWAHUSU NINI?
 
Kama mabadiliko ya kikatiba yaliyofanywa na CCM kwenye mkutano wao wa juzi yana manufaa kwa upande wa upinzani(UKAWA),mbona tangu juzi wapo bize humu JF wanalalamika,au wanaonyesha kasoro na makosa yaliyofanywa na CCM kwenye kikao chao?,si wakae wafurahie tu?,kama waliofukuzwa CCM au wanaofukuzwa CCM wana faida nao si wawakaribishe kwao tu?,mbona wanashinda wanalalamika humu JF?..kana kwamba hawana matatizo ya kutatua kwenye vyama vyao??
 
Acha tu waseme hiyo ndiyo Demokrasia. Kwani hata wakikesha hapa Jf wanaongelea huo mkutano ucku kucha wataidhuru ccm kivipi. ccm ni ileile bhana haitetereki kwa maneno ya mitandaoni. Au vp
 
CHADEMA mnapata wapi ujasiri ya kusema vyama vinginge? Zitto, Mwigamba, Kitila Mkumbo mliwafanya nini? Na vipi wale madiwani 5 wa Arusha? Sasa leo mnaona nongwa kwa CCM kusafisha nyumba yao, au walikuwa watu wenu?
Achana na wajinga hao!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…