Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,961
- 47,828
Kwa mwenye akili, ni dharau kubwa mtu akakuita akasema anataka kuusikia ushauri wako, kumbe mtu huyo alikwishafanya maamuzi yake tayari. Kwa hiyo ushauri wako kwake inakuwa ni kukupotezea muda kwa kuwa alikwishakupuuza. Lakini akaona haitoshi kukupuuza, akataka pia kukuonesha wazi namna anavyokudharau, kwa kutozingatia ushauri wako wote. Hicho ndicho kilichofanywa na CCM, Serikali yake na Bunge lake.
CCM imewafanya watanzania wote hawana maana, hawana akili, hawana haki ya kusikilizwa.
Kwanza Serikali iliwahadaa wananchi kuwa eti inataka kubadilisha sheria ya uchaguzi na ya Tume ya Uchaguzi ili kuongeza demokrasia. Nasema kuwa ni hadaa kubwa kwa sababu miswada hiyo ya sheria haikuwa imejibu malalamiko ya msingi ya wananchi.
Lakini wakaendeleza hadaa kwa kupitisa wabunge wao. Kamati ya Bunge ikawatangazia wananchi kuwa inapokea maoni kuhusiana na miswada miwili ya sheria zinazohusiana na masuala ya uchaguzi. Wananchi wengi kwa kujua umuhimu wa uchaguzi walijitokeza kwenda kutoa maoni yao.
Jambo moja ambalo liliongelewa sana na wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, vyama vya siasa, NGOs na wananchi mmoja mmoja, ni kutaka wakurugenzi wa Wilaya na Halmashauri? ambao kimsingi ni wateule wa Rais, wasiwe wasimamizi wa uchaguzi. Wadau hawa wakashauri Tume ya uchaguzi iwe na watumishi wake kwaajili ya kusimamia uchaguzi. Jambo la pili lililoshauriwa na wadau wengi ni uchaguzi wa Serikali za mitaa kusimamiwa na Tume ya Uchaguzi badala ya TAMISEMI. Na jambo la tatu lililoshauriwa na wadau wengi ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kwa maana ya tangu kuundwa kwake, wajumbe wake na utendaji wake wa kazi.
Maoni haya yote ya wananchi, yamepuuzwa, na miswada wameipitisha kama walivyoiandaa na kupanga bila ya kuzingatia maoni ya wananchi. Hii ni dharau kubwa kwa wananchi wote.
Jambo pekee walilolifanya ni kubadilisha tu jina la Tume ya Uchaguzi eti iitwe Tume Huru ya Uchaguzi. Hii ni sawa muwe na jirani jambazi. Mkawa na malalamiko huyo jambazi aondolewe mtaani penu. Halafu anayetakiwa kumwondoa, badala ya kumwondoa, akasema kwamba huyo bwana kuanzia leo asiitwe jambazi bali aitwe Raia Mwema.
Wito wangu kwa wananchi wote wenye mapenzi mema kwa Taifa letu, anayekupuuza na kukudharau, nawe umfanyie vivyo hivyo. Tuipuuze CCM, tuipuuze Serikali yake, tulipuuze Bunge lake, tuwapuuze na viongozi wao wote.
Waungwana wanasema mheshimu anayekuheshimu. Asiyekuheshimu, anayekupuuza, nawe mtende vivyo hivyo.
Na kuwaonesha kuwa tumewapuuza, tuungane kwenye maandamano yoyote yale yatakayoandaliwa na chama chochote cha siasa au taasisi nyingine yoyote kuikataa miswada hiyo, kuukataa ulaghai wa CCM na taasisi zake. Ndugu wananchi, hawa watu hawatatuheshimu hata siku moja bila ya sisi wenyewe kuwathibitishia kuwa tunastahili na tuna haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa.
Mabadiliko ya sheria, kutoka kwenye sheria mbovu kwenda kwenye sheria bora, kutoka kwenye katiba mbaya kwenda kwenye katiba nzuri, hatuyahitaji kwaajili ya chama fulani au taasisi fulani bali kwaajili ya nchi yetu na jamii nzima ya Watanzania wa leo na kesho.
Wanaotengeneza sheria kwaajili ya kujinufaisha wao binafsi au chama chao au familia zao, ni wahuni, na wahuni hawastahili kuheshimwa wala kusikilizwa. Mungu wetu tunaomba utujalie ujasiri wa kupigania kilicho chema kwa Taifa letu, na katika hilo tunaomba uwe nasi.
Sijawahi kushiriki maandamano ya kudai haki. Safari hii nitashiriki. Nimeamua kushiriki yale yaliyoandaliwa na CHADEMA kule Mbeya. Sitashiriki kama maandamano ya CHADEMA bali kama maandamano ya kupinga hila za watu waovu wasioraka nchibyetu iwe na mifumo mizuri ya demokrasia, utawala na sheria. Ni maandamano dhidi ya wanaoliangamiza Taifa.