Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,961
- 47,828
Ni dhahiri CCM inajitambulisha zaidi kwa uovu kuliko wema, hekima na utu.
Wanaoitwa wabunge wa CCM, asilimia 75, hawakuchaguliwa na wajumbe kwenye kura za maoni. Walitokea wapi, hakuna ajuaye. Uovu wa CCM unaanzia ndani ya chama chenyewe.
Sheria zote mbaya katika nchi hii na katiba mbaya ya nchi hii, vimetengenezwa na CCM.
Umaskini, miundombinu ya hovyo, ukiwemo umeme, na upatikanaji hafifu wa huduma za afya na elimu zenye ubora, vyote vimetengenezwa na CCM. Wakati wanajenga huduma duni za afya, wao wanatibiwa India, South Afrika, USA na Ulaya.
Mifumo hii ya utawala inayowapa uongozi watu corrupt, wanafamilia wao, watu wenye uelewa na uwezo duni, watu wanafiki wasiojua chochote zaidi ya kumsifia Rais, wala rushwa; kwa kupitia njia chafu kama vile kuiba kura, kuwatangaza watu wamepita bila kupingwa baada ya kuwaondoa kwa hila wapinzani wao; vyote hivyo vimeasisiwa, kuendelezwa na kulindwa na CCM.
Hii mifumo ya kuwafanya watawala waogelee kwenye anasa ya utajiri, kwa kuwakamua watu maskini kwa kodi na tozo nyonya damu, kwa kuchukua mikopo mikubwa toka nje isiyo na faida kwa mwananchi, vyote vimeasisiwa na CCM.
Hii mifumo ya kuwatesa, kuwateka na hata kuwaua, kuwafilisi kwa kutumia TRA na hata kuwabambikia kesi wanaokosoa uovu wao, imetengenezwa na CCM na inalindwa kwa nguvu zote na CCM.
CCM leo hii inajitambulisha zaidi kama alama ya uovu, dhuluma, unyonyaji na uchafu wa kila aina, kuliko kujitambulisha kwa wema, haki na hekima.
Hii mifumo inayotoa madaraka yasiyo na mipaka kwa Rais, kiasi cha Rais kuwa na uwezo hata wa kugawa au kuuza rasilimali za nchi kwa namna apendavyo, sawa na nyakati za utawala wa Mobutu kule Zaire, za kuweza kuuza hata ardhi yenye madini, na pesa kuweka kwenye account yake binafsi, yote yameasisiwa na CCM na yanalindwa na CCM kwa nguvu zake zote.
Leo CCM, baada ya kuwadharau wananchi kwa miaka mingi, na malalamiko ya miaka mingi, imefikia hata kuanza kuwaweka kwenye uongozi wa juu wa chama wale wahalifu wakubwa, watuhumiwa wa mauaji, utekaji na upotezaji watu ili wananchi wajue kuwa uovu ule uliokuwa unafanywa na hao watu, ndiyo mambo ambayo CCM kwayo inajivunia na kuyaonea fahari. Hii ni dharau kubwa sana kwa watu wanaopigania na kupenda haki.
Kanuni ipo wazi, anayeonewa, hata kama ni duni kiasi gani, hawezi kuikubali dhuluma. Hata kama CCM ina greenguards, polisi, jeshi, TISS, hivyo haviwezi kuwafanya wananchi wema waache kuupinga uovu wa CCM. CCM imepigwa upofu ili hasira za watanzania zizidi kuwaka dhidi yao.
Nyakati zaja, wananchi watapinga kwa njia zote zinazowezekana, za amani au za shari. Kwa anayeonewa, vyote ni halali.