Kuelekea 2025 CCM imenunua Pikipiki nchi nzima na kuweka nembo ya Samia. Fedha za wastaafu na stahiki za watumishi hazipo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
2,309
1,503
CCM inaendelea kudharau kila kitu na ni dalili wazi kwamba viongozi ndani ya CCM na serikali yake hawana usikivu tena. Ni dharau zilizopitiliza kushindwa kuwalipa watumishi wastaafu pensheni zao na stahiki za watumishi wa serikali huku wakitaabika na kuteseka ilhali fedha za kununua pikipiki na kuzisambaza nchi nzima zipo.

CCM hii inayoishi katika upofu kwa sasa haiwezi kusikia chochote na haijali chochote. Wabunge wakimaliza muda wa bunge wanalipwa fedha zote za kiinua mgongo tena mamilioni ya fedha. Wapo walimu, maaskari, madaktari, manesi na watanzania wote na watumishi wa kada nyingine wanateswa na serikali ya CCM. Hivi kama kweli CCM na serikali yake inaongozwa na watu wenye akili timamu unawezaje kupata nguvu ya kutowalipa watumishi wa kada zote hizo hapo juu?

Je, unawezaje kutengeneza mazingira magumu ya maisha kwa watanzania kila kukicha na ukaendelea kudhani kwamba hawa watanzania wote wanakupenda kwa jinsi unavyowafanyia? Rais Samia na serikali yake watambue kwamba ni muda tu wala si mrefu nchi hii kwa dhambi hizi za viongozi mambo yataharibika. Mnachowafanyia watanzania hata Mungu hapendezwi nacho, mjue hilo.
 
Back
Top Bottom