GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,044
- 119,623
Najua unavyoumia Mdogo wangu ila GENTAMYCINE nasema Watanzania tutakutusi, kukashifu na kukuona huna lolote ila hapo hapo ulipo tambua kuwa Wewe ndiyo Shujaa yetu namba Moja ndani ya Kikosi cha Timu ya Taifa Tanzania ya Taifa Stars.
Najua kuwa Taifa Stars ikifungwa basi Sisi Waswahili tunakutupia lawama zote Wewe ila ikishinda tu kwa Unafiki wetu wa Kutukuka tunakusahau ghafla na kwa muda kisha tunaanza Kuwasifia wengine wanaofunga Magoli ya Kawaida sana ( japo yanasifiwa kuwa ni mazuri ) wakati Wewe umeyafunga hayo sana tu ukiwa TP Mazembe, Genk na Aston Villa na wala hukuwa Mshamba ( Mbwiga ) Kuyashangilia mno kwani una Kipaji na Uwezo pia.
Nakuhakikishia Captain Mbwana Samatta wacha Wanafiki na Waswahili tukuseme sana na tukuone huna Faida wala Msaada wowote kwa Taifa Stars ila nina uhakika kuwa Mguu wako pekee ama Kichwa chako vitatupeleka rasmi na kwa mara ya Kwanza Kombe la Dunia huko QATAR na hapo ndiyo unaenda Kutufunga kabisa Midomo na tutabaki na Aibu zetu huku tukihaha kutaka kuja Kukuomba Radhi ( Msamaha ) kwa yote.
Tuvumilie tu Captain Wetu na tuzoee!!!!