Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,181
- 5,553
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amebaini Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limepata hasara ya Sh894 milioni licha ya kupokea ruzuku ya Sh4.55 bilioni kutoka serikalini.
Hata hivyo, hasara kwa shirika hilo imepungua kwa asilimia 94. CAG amesema shirika hilo limerejesha Sh4.4 bilioni kutoka kwenye ruzuku hiyo kama mapato yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
CAG Kichere amesema hayo leo Machi 28, 2024 wakati akiwasilisha taarifa yake ya ukaguzi kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.