C. TAWALA FC TUBADILISHE KOCHA. HALI SIYO NZURI TENA

Auto-Marvelt

JF-Expert Member
Jul 13, 2019
1,741
3,461
Niweke wazi kwanza, mimi sio timu Tawala wala Tawaliwa bali timu maendeleo.
Kila kukicha tunaona makundi yanaibuka yanayosema kocha wetu anaupiga mwingi hadi unamwagika lakini bahati mbaya ni makundi ya wachezaji tu sio mashabiki.
Kocha anashindwa kufanya sub-konki za kutupa alama tatu badala yake anatoa bonus kwa wachezaji tu na mbaya zaidi anachukua wachezaji wa nje kwa mkopo ambao sisi mashabiki ndio tunapaswa kuwalipa wakati hawatunufaishi.
Timu za nje zinatusaidia wachezaji kibao hadi sasa wamefika 97 lakini hatuoni dalili ya kuwanufaisha mashabiki.
Namna alivyopatikana kocha kiukweli mashabiki hatukuelewa maana sio kawaida ya timu yetu mbaya zaidi tunavyowafanyia figisu timu pinzani ndivyo tunazidi kuwapa nguvu zaidi tunahisi tunaididimiza timu yao kumbe tunajenga, tunaipitisha dhahabu kwenye moto na ligi ikifika patamu zile cheche za moto si ajabu zikatuunguza sisi.
Uwezo wa kocha wetu unaweza kuwa ni mzuri ila wachezaji wanampamba hadi kwenye mambo madogo na ya kawaida. Tumesahau kama mbinu nyingi na facilities tunazomsifia ni maono ya kocha aliyepita.
Leo hii kocha wao amefungiwa na Fifa lakini mashabiki wengi wa mpira wanahisi kocha wetu kahusika na wanalaumu sana kwani benchi letu la ufundi limetanda sehemu zote ili kuhakikisha mpira haumfikii kocha wao asije akajiongezea idadi kubwa ya mashabiki.
Ni vyema TUBADILISHE KOCHA kabla mambo hayajaharibika
Tuipende timu kwanza kabla ya kumpenda kocha.
 
Niweke wazi kwanza, mimi sio timu Tawala wala Tawaliwa bali timu maendeleo.

Kila kukicha tunaona makundi yanaibuka yanayosema kocha wetu anaupiga mwingi hadi unamwagika lakini bahati mbaya ni makundi ya wachezaji tu sio mashabiki.

Kocha anashindwa kufanya sub-konki za kutupa alama tatu badala yake anatoa bonus kwa wachezaji tu na mbaya zaidi anachukua wachezaji wa nje kwa mkopo ambao sisi mashabiki ndio tunapaswa kuwalipa wakati hawatunufaishi.

Timu za nje zinatusaidia wachezaji kibao hadi sasa wamefika 97 lakini hatuoni dalili ya kuwanufaisha mashabiki.

Namna alivyopatikana kocha kiukweli mashabiki hatukuelewa maana sio kawaida ya timu yetu mbaya zaidi tunavyowafanyia figisu timu pinzani ndivyo tunazidi kuwapa nguvu zaidi tunahisi tunaididimiza timu yao kumbe tunajenga, tunaipitisha dhahabu kwenye moto na ligi ikifika patamu zile cheche za moto si ajabu zikatuunguza sisi.

Uwezo wa kocha wetu unaweza kuwa ni mzuri ila wachezaji wanampamba hadi kwenye mambo madogo na ya kawaida.

Tumesahau kama mbinu nyingi na facilities tunazomsifia ni maono ya kocha aliyepita.
Leo hii kocha wao amefungiwa na Fifa lakini mashabiki wengi wa mpira wanahisi kocha wetu kahusika na wanalaumu sana kwani benchi letu la ufundi limetanda sehemu zote ili kuhakikisha mpira haumfikii kocha wao asije akajiongezea idadi kubwa ya mashabiki.

Ni vyema TUBADILISHE KOCHA kabla mambo hayajaharibika

Tuipende timu kwanza kabla ya kumpenda kocha.

ahsante sana

Unajua maana ya Paragraphs kwenye bandiko lolote lile
 
Gentleman,
vibaka na matepeli wa siasa pamoja na waropokaji awae wowote nchini,
hawataruhusiwa kamwe kuandaa uhalifu, kufanya ujambazi wao, wizi, utapeli, fujo ama ghasia sehemu yoyote nchini.

na kwasabb hiyo basi,
ni wazi CCM itaitawala na kuongoza serikali ya kizalendo Tanazania mpaka ukamulifu wa dahari,

ni muhimu zaidi kuhusu hilo muarifiane nyote na bila kumficha Mwenyekiti wa chama chenu Taifa 🐒
 
🚮🚮
 
mi naona mashabiki tungebadili timu kwanza hata kwa misimu kadhaa.

mashabiki wengi wa man u,, hapa kati wamejishikiz timu kadhaa kwanza kupata hata japo lepe la furaha ----- mbinu hii ihamie hapa kwetu kama malalamiko ya mada mezani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…