Bunge litoe hoja ya ifanyike AUDIT Ujenzi wa miundombinu Chato

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kumekua na malamiko mengi sana miongoni mwa jamii kua kuna kasi isiyokukua ya kawaida ya Ujenzi wa miundombinu katika mji wa Chato kuliko miji mingine midogo nchini, miundombinu inayolalamikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chato, Ujenzi wa Jengo la TRA linalosemekana kukadiriwa kua na ghorofa mbili au zaidi, Ujenzi wa kituo Cha polisi linalosemekana kukadiriwa kua na ghorofa mbili na zaidi, pia kuna mpangilio wa taa za babarani "Traffic lights" ambazo hata kajika mji wa jirani katoro hakuna.

Kufuta malalamiko haya juu ya serikali ambayo imekua ikipigia kelele suala la rushwa, tuliombe bunge letu endapo mbunge yeyote atapeleka hoja ya kulitaka bunge kumwagiza mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG afanye ukuguzi ili kubaini ukiukwaji wa taratibu za sheria ya manunuzi au laah, je hata utangazwaji wa zabuni ya mkandarasi wa miradi hiyo ulizingatia vigezo.Hilo likifanyika na majibu sahihi yakapatika basi nafikiri mjadala juu ya maneno maneno kwa Rais wetu mpendwa yataisha.Yafanyike kupitia bunge la vikao vijavyo na ikiwezekana hata kamati ya PAAC ifanye hiyo kazi.

Hatukatai kuhusu kuboresha miundombinu ya nyumbani kwa mkuu wetu wa nchi lakini pia ili kuondoa sintofahamu juu ya hilo ni bora haya yakafanyika, hii ndio busara itakayoendana falsafa ya hapa kazi tu.Kunapokua na hofu juu ya kitu flani inapendeza sana ukweli ukajulikana.

Sikumbuki ni lini mzee wetu mtstaafu aliwahi hata kupanga taa za kutosha pale katika mji wetu wa masasi, maana huo mji majengo yake ya TRA na Kituo cha polisi ni nyumba za kawaida tu, hakuna kiwanja cha kimataifa pale masasi labda cha Chopa pamoja na mji huo kua na kasi kubwa ya maendele kulinganisha na wilaya zingine za mikoa ya kusini.

Tukumbuke kua mzee wetu ndiye mwenye mamlaka ya kuamua chochote, Pesa zote za umma ziko chini ya mamlaka yake! Hivyo watu wanaposikia maneno Kama haya unakua ni mshtuko na sintofahamu kwenye jamii! Hivi inawezekanaje Mkuu wetu anayechukia vitendo vya rushwa akamweka ndugu yake kama PS wizara ya fedha? Tutalikwepaje lile neno "CONFLICT OF INTEREST" kwenye jambo kama hili?

Binafsi moyo Wangu bado unasita kuamini haya mpaka pale CAG atakapoamua kukagua na kuuambia umma kinachojiri kile. Je, kuna ukweli wowote? Wanaolalamika wana ushahidi?Mimi na wewe hatumjui, zipo mamlaka husika kushughulikia hayo mambo.

Duniani kote bunge ndio mhimili muhimu sana unaoweza kuamua hatima ya taifa lolote lile, bunge ndio mhimili pekee wenye meno ya kudhibiti mienendo flani ya viongozi wa mataifa hayo. Bunge pekee ndio lenye mamlaka kuunda utawala wa taifa pekee kuliko mhimili wowote duniani kote.
 




Mbona siye atujalalamika jamii gani unazungumzia .
 
watanzania ni wanafiki sana mtu akijenga kwao tatizo, asipojenga baadae mtasema hakufanya kitu chato mpaka ameondoka, mimi naona ajenge tu ikibidi chato ifike mbali zaidi ya hapo
 
Hivi kwasasa ofisi ya CAG itakuwa imesalimika? kwa maana Judiciary tu iko katika hali ya sintofahamu,ilhali ni moja ya mhimili katika uongozi wa inchi.Je ofisi ya CAG itakuwa bado inafanya kazi zake kwa uhuru?
 

Kumbe anajenga polisi na TRA. Mimi nilifikiri anajenga nyumba zake na kuweka taa kwenye nyumba zake.
Ukiona CHATO kumependeza uhamie chato tu.
 
Mtoa mada Kwanza naomba unijuze bunge lipi? Hili la kina maji marefu na kina nanii yule mbunge wa ulanga?
 

haitawezekana kwa sababu wabunge ambao likely wangefanya ivo either wana kesi za kutunga tunga mahakaman so wamewekwa bize uko with same liking of gestapo kind of evidence during german nazi rule, wengine pia wamefungwa kwa shoddy evidence izo izo, au wengine wamekimbia nchi kuhofia maisha yao au wengine kutokana na sheria kandamizi ya cybercime na media bill ni ngumu wamefungwa mikono na mdomo kabisa hata wachambuz huru kwenye mitandao ya kijamii nao mwendo ni ule ule obvious huwez tegemea mbunge wa ccm akathubutu kuhoji wako pale kukusanya posho zao na kupitisha miswada tu ya serikali pendwa hii.

so ile slogan ya acha tuisome namba itaendelea ku apply for a while for now.........
 
Mtoa mada Kwanza naomba unijuze bunge lipi? Hili la kina maji marefu na kina nanii yule mbunge wa ulanga?
Hilo hilo mkuu! Waangalie maslahi ya taifa kwanza, vyama baadae.
 
Hivi huwezi ukawa mbunge ukategemea mshahara wako na posho ukaishi? Ukiwa na mawazo yenye kujenga taifa utafukuzwa uanachama kwa kuusema ukweli?
 
Anajenga ikulu chato...

Acha upumbavu .........

Na utoto na propaganda......

Nonsense........
Ungeachana nao hawa mkuu maana hata faida hawana, mara nyingi watu wa aina hii maisha hua magumu sana ya kuunga unga
 
Hivi kwasasa ofisi ya CAG itakuwa imesalimika? kwa maana Judiciary tu iko katika hali ya sintofahamu,ilhali ni moja ya mhimili katika uongozi wa inchi.Je ofisi ya CAG itakuwa bado inafanya kazi zake kwa uhuru?
Kisheria ukisoma katiba kumsimamisha CAG kazi ni ngumu sana.
 
Halafu majengo ya serikali ambayo ni kama ikulu ndogo,yako kwenye shamba la ukoo,kwa nini yasingetafutiwa kiwanja kikawa na hati ya serikali kwa kuwa zinazotumika ni fedha za umma,siku wanaukoo wakiamua kugawana mali, hayo majengo yatakwenda wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…