Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Halima Mdee, amewasilisha taarifa ya kamati hiyo mbele ya Bunge inayoonyesha mapungufu makubwa kwenye Halmashauri nyingi nchi kushindwa kukusanya mapato ya Serikali.
Mbunge Halima Mdee, akizungumza katika mjadala wa Taarifa za Kamati za PAC na LAAC kuhusu Ripoti ya CAG, ameeleza kuwa mapato ya Tsh. Bilioni 61.15 hayajakusanywa kutoka vyanzo muhimu. Mdee alitaja Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuwa miongoni mwa wazembe, ikishindwa kukusanya fedha kutoka kwa Mkandarasi wa Ujenzi wa Reli ya SGR, Yapi Merkezi.
View attachment 3138273