Bunge laahirishwa ghafla tena, Wabunge 11 wa Upinzani wahojiwa na Kamati ya Maadili

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,660
55,492
Waziri wa Nishati na madini George Simbachawene alipoanza kusoma kwa mara ya pili Muswada wa mafuta na gesi asilia(Muswada juu ya Petroli, 2015 The Petroleum Act, 2015), Tundu Lissu alisimama na kuomba Kuhusu utaratibu, Spika hakumpa nafasi, ndipo wabunge wote wa UKAWA Waliposimama na kuanza kupiga kelele wakisema Muongozo muongozo..!!.

Spika Kamuomba Waziri aliyekuwa anasoma Hotuba akakae kisha akawataja baadhi ya wabunge kwamba ndio wanaoleta fujo bungeni kwa kosa kutokana na kanuni ya kuleta fujo bungeni ambao ni:

1.John Mnyika Mbunge wa CHADEMA jimbo la Ubungo

2.Tundu Lissu Mbunge wa CHADEMA jimbo la Singida Mashariki

3.Ernest Silinde Mbunge wa CHAEMA jimbo la Mbozi Magharibi

4.Rashid Ali Abdalla mbunge wa CUF jimbo la Tumbe Zanzibar

5.
Paulina Gekul Mbunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA wa Mkoa wa Manyara

6.
Moses Joseph Machali Mbunge wa NCCR-Mageuzi Jimbo la Kasulu Mjini

7.
Rajab Mbarouk Mbunge wa CUF Jimbo la Ole Zanzibar

8.Felix Francis Mkosamali Mbunge wa NCCR Mageuzi jimbo la Muhambwe

9.Rev. Simon Peter Msigwa Mbunge wa CHADEMA jimbo la Iringa Mjini

10.Joseph Roman Selasini Mbunge wa CHADEMA jimbo la Rombo

11.Khalifa Suleiman Khalifa Mbunge wa CUF Jimbo la Gando Zanzibar

Bunge limesitishwa hadi watakapoitwa tena na Spika, vilevile kamati ya Maadili imeitwa kujadili hili Swala.


Bonyeza HAPA kumsikiliza Spika alichokisema Bungeni



Kufuatia Vurugu zilizotokea leo Bungeni, Kamati ya Maadili inawahoji wabunge 11 wa upinzani kwa vurugu zilizopelekea Bunge kusitishwa leo wakati miswada ya petroli, gesi ikiwasilishwa.

Leo asubuhi wabunge wa Upinzani walisimama wakati Waziri wa Nishati na Madini anasoma Muswada wa Mafuta na Gesi Asilia, ili kushinikiza Waziri asisome Muswada wa Mafuta na Gesi ambao umeletwa Bungeni kwa Hati ya Dharura.

Wabunge wa Upinzani wanapinga hatua hiyo wanadai Muswada Mkubwa kama huu uliobeba maslahi makubwa ya Taifa hautakiwi kupelekwa haraka, unahitaji muda wa kutosha wa wadau na Wabunge kuupitia ili kurekebisha mapungufu yaliyopo.

Baadhi ya Wabunge wanadai Muswada ni Copy and Paste kutoka kwenye Muswada wa Mafuta wa Nchini Uganda.
 

Attachments

  • bungeni2.mp3
    1.5 MB · Views: 17,199
Watu wameshachukua hela za watu alafu nyie mnaleta umbea,hao jamaa watapigwa ban bungeni na miswada itapitishwa faster...sisi tunataka kusign kabla hatujatoka madarakani alafu nyie mnaleta kelele p.u.m.b.a.f.
 
Kwani Ni Lazima Miswaada Hii Ipitishwe Kwa Sasa. Kuna Uharaka wa Nini Kwenye Maswala Nyeti Kama Haya. Nadhani Tujipe Muda Ili Sheria za Gas na Mafuta Zitakazokuwa zimepitishwa ziwe na Manufaa zaidi Kulikoni Kulimbilia as if ndio Mwisho wa Kutunga sharia.

Kawia ufike, Ni kheri Tuchelewe Kuipata sharia Hiyo ila Tukishaipata Basi Iwe neema kwa Tanzania na Watanzania.
 
Serekali ipo kwa niaba ya wananachi. Miswada, sheria inapaswa i serve interest za wananchi. Upinzani kazi yake ni kuikosoa serekali pale isipotekeleza or serve interest za wananchi. Sheria, zinapaswa zipelekwe zenye maslah ya wananchi, bunge likae kiutaalamu na kutengeneza sheria iliyo bora kwa nchi, wapinzani na chama tawala wote inapaswa watoe mutual and beneficial laws for citizens welfare. What is happening? Kwenye current parliament. Tujiulize, tuko sawa ? Wapi tumeshindwa ?, yapi ni maziri?, Nini kifanyike.
 
Huo muswada wa gesi wanataka kumfurahisha Obama wapinzani msikubali huo upuuzi kuendelea hapo bungeni.
 
Kwani Ni Lazima Miswaada Hii Ipitishwe Kwa Sasa. Kuna Uharaka wa Nini Kwenye Maswala Nyeti Kama Haya. Nadhani Tujipe Muda Ili Sheria za Gas na Mafuta Zitakazokuwa zimepitishwa ziwe na Manufaa zaidi Kulikoni Kulimbilia as if ndio Mwisho wa Kutunga sharia.

Kawia ufike, Ni kheri Tuchelewe Kuipata sharia Hiyo ila Tukishaipata Basi Iwe neema kwa Tanzania na Watanzania.

Washakula amana watailipaje.
 
Back
Top Bottom