Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,901
- 1,335
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Mhe. Hassan Mtenga, amemuagiza Mshauri Elekezi wa ujenzi na maboresho wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kufanya maboresho ya hospitali hiyo ili iendane na ramani za kisasa na kuwa na mwonekano unaovutia, lengo likiwa ni kukuza sekta ya afya na kuvutia zaidi watalii wa tiba.
Akizungumza baada ya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo, Mhe. Mtenga amesisitiza umuhimu wa hospitali hiyo kuwa ya kisasa ili kuongeza thamani ya huduma zinazotolewa.
“Tunataka hospitali hii iwe ya mfano si tu kwa huduma za kibingwa, bali pia kwa mwonekano wa nje na ndani. Maboresho haya si anasa ni mkakati wa kuboresha sekta ya afya na kuvutia zaidi watu kuja kutibiwa hapa,” amesema Mhe. Mtenga.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema Mkoa wa Mara una fursa kubwa ya kuwa kivutio cha utalii wa tiba kutokana na jiografia yake kwani Hospitali hiyo, inaweza kuvutia wagonjwa kutoka Kenya, Uganda, na hata nchi nyingine jirani kuja kutibiwa
Kwa sasa, ujenzi wa awamu ya tano ya hospitali hiyo unaendelea, ikiwa imefikia asilimia 15, huku kukiwa na mpango wa kukamilisha majengo yote, kusimika mitambo ya kisasa, na kuimarisha miundombinu ifikapo mwaka 2025. Hospitali hiyo tayari inatoa huduma za kibingwa kama vile upasuaji, radiolojia, huduma za watoto njiti (NICU), na usafishaji damu (dialysis), na imeanza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa mkoa huo na maeneo jirani.