Bunge la 12 Mkutano wa 19 Kikao cha 2 April, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
4,089
13,932
Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 unaendelea leo Aprili 9, 2024 Jijini Dodoma ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atasoma hotuba ya bajeti ya ofisi yake na taasisi zake kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026.

Taarifa mbalimbali za kamati za kudumu za Bunge nazo zitawasilishwa ikiwemo; Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na maoni ya kamati kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Nyingine ni taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na maoni ya kamati kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mfuko huo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na maoni ya kamati kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Wabunge pia watauliza maswali kwenda kwenye wizara mbalimbali.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema Serikali imejipanga kikamilifu kupambana na kudhibiti rushwa katika kipindi hiki cha Uchaguzi ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi kuhusu vyanzo vya Mapato ya Wagombea, Wapambe wao na Vyama vya Siasa ili kudhibiti matumizi ya fedha haramu, kuchunguza na kuwachukulia hatua za Kiseria Wagombea na Wapambe watakaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2025.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitoa hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu na Bunge 2025/2026

"Serikali imeendelea kubuni na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuzalisha fursa za ajira nchini kupitia uwekezaji na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki, reli ya kisasa, Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato. Vilevile, Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kukua na kupanua wigo wa uzalishaji wa ajira nchini. Kutokana na jitihada hizo, katika kipindi cha Novemba 2020 hadi Februari, 2025 jumla ya ajira 8,084,204 zimezalishwa katika sekta ya umma na sekta binafsi."

"Katika kipindi cha Agosti Mosi 2024 hadi Februari 2025, jumla ya Shilingi Bilioni 54.9 zimekusanywa kupitia huduma ya usafiri wa reli kati ya Dar es Salaam – Morogoro – Dodoma. Ameeleza kuwa katika kipindi hicho, jumla ya abiria 1,809,983 wamesafirishwa kupitia huduma hiyo ya reli.

"Uwepo wa huduma hiyo ya treni, umepunguza muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma kutoka wastani wa saa 10 kwa basi hadi kati ya saa tatu na nne na kuchagiza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini,"

Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa ambapo hadi Februari 2025, ujenzi wa kipande cha Mwanza–Isaka (km 341) umefikia asilimia 62.37, Makutupora–Tabora (km 368) asilimia 14.53, Tabora–Isaka (km 165) asilimia 6.33, na Tabora–Kigoma asilimia 7.3. Majaliwa ameongeza kuwa maandalizi ya ujenzi wa kipande cha Uvinza–Malagarasi–Musongati (km 282) yameshaanza baada ya Tanzania na Burundi kusaini mkataba wa ujenzi wa reli hiyo mnamo Januari 29, 2025.

"Serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme katika Bwawa la Julius Nyerere kwa gharama ya shilingi trilioni 6.6. Ujenzi wa mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 kwa siku umekamilika. Hadi Machi 2025, jumla ya megawati 2,115 zimeunganishwa kwenye gridi ya taifa na hivyo kuongeza kiwango cha umeme katika gridi ya taifa kufikia megawati 4,031.7. Kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika mradi huo kumeongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuwa chachu ya kasi ya maendeleo ya nchi."

"Kwa kuzingatia ushindani wa kibiashara uliopo katika ukanda wa Bahari ya Hindi, nchi yetu imechukua hatua mahsusi ili kunufaika na fursa ya kijiografia tuliyonayo ya kuwa lango kuu la kibiashara kwa nchi jirani. Hatua hizo ni pamoja na uboreshaji wa bandari zetu zilizo katika Bahari kuu na uwekezaji wa sekta binafsi katika kutoa baadhi ya huduma bandarini"

"Vilevile, mapato ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kwa mwezi yameongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 mwaka 2023/2024 hadi kufikia wastani wa shilingi trilioni moja mwaka 2024/2025. Aidha, mapato yanayokusanywa kutokana na ushuru wa forodha yameongezeka kutoka shilingi trilioni 9.35 mwaka 2023/2024 hadi shilingi trillioni 9.86 kufikia Februari 2025."

"Jumla ya miradi 1,633 imetekelezwa, ambapo miradi 1,335 ni ya vijijini na miradi 298 ni ya mijini. Miradi hiyo imeongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka wastani wa asilimia 70.1 mwaka 2020 hadi asilimia 79.6 mwaka 2025."

"Kwa upande wa mijini, kiwango hicho kimeongezeka kutoka wastani wa asilimia 84 mwaka 2020 hadi asilimia 90 mwaka 2025. Kutokana na ongezeko hilo, wananchi wapatao 12,547,526 wamenufaika na huduma ya maji"
 

Attachments

  • sw_1744092373_HOTUBA_YA_WAZIRI_MKUU_WA_JAMHURI_YA_MUUNGANO_WA_TANZANIA.pdf
    4.7 MB · Views: 1
Kikao cha maccm hiki hakina issue.

No reforms no election, ndiyo habari ya mjini.
 
Uchaguzi gani unauongelea simbachawawene?
Si mpo pekeenu? Uchaguzi wa nini kupoteza muda.
Pendekezaneni majina apishaneni tuendelee na maisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom