Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,934
- 13,689
Bunge la 12 Mkutano wa 18 kikao cha 8 Januari 6, 2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia Sera za nje na kuimarisha mahusiano mazuri na mataifa mengine huku ikijikita zaidi katika kujitegemea kiuchumi.
"Ni muhimu kuzingatia Sera za nje. Rais Samia ameendelea kuifanya nchi hii kuwa na mahusiano na mataifa mengi duniani. Marekani ni moja kati ya nchi hizo. Muhimu kwetu, pamoja na upana huu wa mahusiano, ni kuhakikisha tunajiimarisha na kuwa na uwezo wa ndani wa kutekeleza mipango yetu. Bajeti zetu zinapaswa kumudu sekta zote muhimu kama afya, elimu, na maji, pamoja na maeneo mengine tuliyokubaliana na mataifa husika."
"Kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha tunashirikiana na kutumia rasilimali tulizonazo kujenga uchumi wa ndani," alihitimisha Waziri Mkuu.
"Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tunakaribisha uwekezaji mkubwa kwenye mazao haya ikiwamo parachichi ili yaweze kwenda mahali, huku tukiyaongezea thamani."
"Tunapozungumzia kwenye ajira, Serikali nayo inawaangalia sana wanawake, pale ambapo kunakuwa na ushindani wa mwanamke na mwanaume, basi nafasi ya kwanza anapewa mwanamke. Hayo ni malengo ya Serikali ya kufikia 50/50."