Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 6 Februari 4, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,935
13,691
Wakuu

Wabunge leo katika kikao chao cha sita katika mkutano wa 18, baada ya Kipindi cha Maswali na Majibu, watapokea na kujadili Taarifa za Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii pamoja na Kamati ya Afya na Masuala ya UKIMWI.

Kamati hizo zinatarajiwa kuja na maazimio pamoja na maoni mbalimbali kwa serikali kutokana na shughuli zake kwa mwaka uliopita 2024.


Serikali imeahidi kutuma vifaa tiba na wataalam katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Kata ya Mabogini, ili wananchi waanze kunufaika na huduma. Ahadi hiyo ilitolewa baada ya Mbunge Prof. Patrick Ndakidemi kuuliza kuhusu mipango ya serikali ya kupeleka vifaa na wataalamu hospitalini hapo. Naibu Waziri wa Afya, Festo Dugange, alikishukuru jimbo hilo kwa juhudi za kumaliza ujenzi wa hospitali, akisema serikali imetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba ili huduma zianze haraka.

Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu ameishauri serikali kuwawezesha vijana kiuchumi ili kuepukana na ngono zembe zinazosababishwa na matumizi mabaya ya pombe, wakati akichangia Taarifa za Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, na Kamati ya Afya na Masuala ya UKIMWI.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu - Patrobas Katambi

Serikali ya Tanzania imeanzisha riba kwa mifuko ya hifadhi ya jamii itakayosababisha ucheweshaji wa mafao kwa wanachama huku Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ukilipa asilimia 15 wakati Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) utalipa asilimia tano, alipokuwa akijibu swali la msingi la mbunge wa viti maalumu (CCM), Fakharia Shomar Khamis.

Katika swali la msingi, Fakharia amehoji iwapo mstaafu aliyecheleweshewa kupata mafao anaweza kudai fedha kutokana na usumbufu alioupata wakati anasubiri mafao yake.

Akijibu swali hilo, Katambi amesema Sheria za NSSF na PSSSF katika vifungu 49(3) na 43(3) mtawalia, vinaeleza endapo mfuko utachelewesha kulipa mafao kwa mwanachama na uchelewesho huo haukusababishwa na mwanachama mwenyewe au mwajiri, utalipa riba.

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema ubadilishaji wa majina ya kampuni hauna athari kwenye mchakato wa ukusanyaji kodi kwani namba ya utambulisho wa mlipakodi huwa ni ile ile.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, amesema hadi Januari 2025, Serikali kupitia REA imekamilisha upelekaji umeme katika vijiji vyote 12,318, na sasa inasambaza umeme vitongojini. Akijibu swali Bungeni, alieleza kuwa umeme umefika katika vitongoji 33,657 kati ya 64,359 (52.3%), huku vitongoji 30,702 vilivyobaki vikihusishwa kwenye miradi ya muda wa miaka 5-10 kuanzia 2023/24.

Pia, vitongoji 4,020 vipo kwenye mpango wa utekelezaji. Kwa Wilaya ya Kilindi, maeneo 4 kati ya 12 ya uchimbaji dhahabu yamepata umeme, huku mkandarasi akishughulikia eneo la Matanda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom