Bulaya Atamba Kumshinda Wassira

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mbunge wa Bunda Mjini, mkoani Mara, Esther Bulaya (Chadema), ametamba kuwa ataendelea kumshinda mpinzani wake kisiasa, Stephen Wasira (CCM), kwa madai kwamba alipata ubunge huo kihalali.

Bulaya alisema hayo jana ikiwa ni siku moja tangu kutupwa kwa rufaa ya wanachama wa CCM waliokuwa wakipinga ushindi wa mbunge huyo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 dhidi ya Wassira na wagombea wa vyama vingine.

Mbunge huyo aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake kuwa, alimshinda Wasira kwa wananchi, akamshinda kisheria, lakini hakuridhika akakata rufaa na ameendelea kumshinda.

"Kama ana mpango wa kukata rufaa nyingine aende akate tu, lakini akumbuke kuwa nitaendelea kumshinda tu kwa sababu ubunge wangu sio wa kuchakachua bali nimeupata kutokana na kura za wananchi wa Bunda Mjini," alisema Bulaya na kuongeza:

"Siku zote nimekuwa nikisema kuwa waliofungua kesi sio wanachama wa CCM bali ni Wasira mwenyewe, ndio maana akawa mkali kupigwa picha na waandishi ili Watanzania waendelee kudhani kwamba hayumo katika kesi hiyo," alisema.

Alisema wakati umefika sasa mwana siasa huyo mkongwe kupumzika na kula mafao yake, kwa kile alichosema ametumikia taifa kwa muda mrefu na sasa ni zamu ya wengine kumpokea kijiti ili kuanzia pale alipoachia.

"Pamoja na hayo ninamkumbusha kuwa siku zote mahakama husimamia haki ndio maana ameshindwa mara mbili katika kesi hii, hivyo hana budi kupumzika," alisema.

Januari 25 mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitupilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na wapigakura Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagira kupinga ubunge wa Bulaya.

Bulaya alihama CCM na kujiunga na Chadema katikati ya mwaka jana na kuteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini na kufanikiwa kumbwaga mkongwe huyo kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
 
Duh! Siasa haifai kabisa. Yaani ukikumbuka jinsi Wassira alivyokuwa mtu muhimu kwenye serikali ya JK halafu ukalinganisha na alivyofubaa kwenye awamu hii ya Magufuli, utakata tamaa kabisa kujiingiza kwenye siasa.
 
Duh! Siasa haifai kabisa. Yaani ukikumbuka jinsi Wassira alivyokuwa mtu muhimu kwenye serikali ya JK halafu ukalinganisha na alivyofubaa kwenye awamu hii ya Magufuli, utakata tamaa kabisa kujiingiza kwenye siasa.
Na huyo mzee kwa kufubaa ni balaa, nakumbuka kipindi ameeenda NCCR biashara zake zilikwama akawa kama msukule ukimuona barabarani, nishawahi kutana naye mahali kipindi akifuatilia leseni ya biashara yake ya samaki.....dah....nilikoma alivyokuwa amechoka, ingekuwa ndio kipindi hichi wallah ningepiga naye selfie.......ss kama amefubaa tena kwa muda mfupi namna hii, nadhani kuna shida mahali.
 
Duu hivi hakunaga cha kufanya ni ubunge na uwaziri tuu na unalazimishaje kuwaongoza watu walikukataa yaani ukishona mtu ana mtumbo mkubwa ni wa kumuogopa Santa.liende kule bana tumeshalichoka halina hata watoto wanapita huku walifikishie ujumbe y
 
Yaani mimi aliniudhi saaaana jinsi alivyoikomalia katiba ya Chenge na kuipuuzia rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba. Waliobaki kwenye system waliokuwa na kimbelembele cha Katiba ya Chenge ni Lukuvi, Simbachawene na Kairuki.
 
Duh! Siasa haifai kabisa. Yaani ukikumbuka jinsi Wassira alivyokuwa mtu muhimu kwenye serikali ya JK halafu ukalinganisha na alivyofubaa kwenye awamu hii ya Magufuli, utakata tamaa kabisa kujiingiza kwenye siasa.
Unahukumiwa sawasawa na makosa yako
 
Esta Mwanamke wa shoka aliempumzisha wasirra baada ya walioba kumshindwa Tyson wa TZ
 
JPM mteue Wasira angalau awe DC.
Atakufa njaa,sasa hivi ana hali mbaya.
 
Mtuachie Wassira wetu. Tulimpiga chini ili tujue sifa yake upande wa pili. Tuko hapa Bunda mjini na mbunge wetu Easter akisikiliza matatizo ya wananchi. Karibuni sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…