Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 26,084
- 62,774
Habari Wakuu!
Nimetembea tembea kidogo kwenye nchi yetu hii.
Hivi ni kusema Watu kutoka Kagera, Arusha, Moshi na Mbeya ndio wanayoichangamsha miji mingi ya Tanzania?
Maana ikifika mwezi wa 12 hasa kuanzia tarehe 20 mpaka tarehe 1 January hawa watu wakienda kwao miji mingine yote hupoa kama uji.
Hakuna cha Dar es salaam,
Hakuna cha Mwanza,
Hakuna cha Kahama,
Hakuna cha Mafinga wala Makambako,
Hakuna cha MOROGORO
Hakuna cha Katoro,
Hakuna cha korogwe,
Miji yote hiyo huwa Kimya msimu huu. Wakati ni miji iliyochangamka Sana kipindi kisicho na sikukuu za miisho ya mwaka.
Kuchangamka Kwa miji hapa nazungumzia wingi wa watu barabarani au kwenye maduka, wingi wa foleni ya magari, mbwembwe za sherehe na shughuli za hapa na pale, vifo vya ng'ombe, Mbuzi na kuku, nguruwe na wanyama wengine.
Miji ya Kagera, Arusha, Mbeya na Moshi mingi msimu huu hupamba moto kuliko ilivyokawaida.
Kuna watu watanibishia na kuona naongea na sijatembea.
Labda watasema nao mbona wanafurahia sikukuu tuu Kama kawaida lakini niwaambie tuu Maeneo niliyoyataja hapo juu yaani Kagera, Arusha, Moshi na Mbeya msimu huu wakati Maeneo mengine yakinunua nyama Kwa kilo wao wanaangusha NG'OMBE au Mbuzi kadhaa, huku kuku wakihesabiwa sio nyama kwani watachinjwa wengi Kama kumbikumbi.
Wakati Maeneo mengine yakinunua pombe Kwa chupa Moja Moja, Maeneo tajwa hapo juu yaani Kagera, ARUSHA, Moshi na Mbeya watanunua Makreti Kwa makreti ya Bia huku pombe za kienyeji zikihesabika Kama Juisi tu.
Sherehe na shughuli za hapa na pale ni nyingi Maeneo tajwa hapo, watu wanaenjoi na kusahau shida zao, watu hawaionei huruma pesa kwani waliitafuta wenyewe, watu wanafurahia kuishi Duniani wakiwa nchi Yao yenye Amani.
Pika mapilau ita mtaa mzima wekeni sherehe kuleni pamoja, wekeni muziki, andaeni programu Vijana wawaburudishe Kwa Ngoma, nyimbo na jambo lolote. Msizubae zubae Kama wanyama.
Kwa mwanadamu hakuna zaidi ya Kula na kunywa na kufurahi. Huko kuzimu hakuna mambo hayo ndugu zangu. Na Kama ni kukaa tutakaa Sana kuzimu. Embu angalia aliyekufa miaka ya 1950 huko mpaka Leo bado yupo kuzimu. Usidanganywe kuwa ukifa utafufuka kufumba na kusumbua😀😀😀 .
Tufurahini, tujumuike ndugu, jamaa na marafiki. Wenye pesa Kwa wasio na pesa. Wenye pesa watatoa chakula na vinywaji, wasio na pesa watatoa nguvu zao kujiandaa, wenye vipaji watatuburudisha tusio na vipaji, tutawasifia Sisi nasi tukiburudika. Tusizubae zubae ndugu zangu.
Kifo kikija kitatufungia kuzimu muda mrefu Sana.
Juzi nilikuwa Arusha na Moshi, miji imechangamka mno, Jana mapema nilikuwa Morogoro, kumepoa nikasema hapa hapanifai Acha nije DAR. Nafika huku nako naona kumepoa Sana hakuna shangwe zozote zaidi ya mingurumo ya Mwendokasi tuu shenzi!
Hapa nimeshakata ticket ya Ndege ya Bukoba, jioni Kama saa 11 nitakuwa Kwa Wahaya Huko najua hawataniangusha.
Sasa nijibiwe!
Hivi miji mingine ya Tanzania mnashindwaje kufurahia Maisha hasa misimu ya sikukuu Kama hizi?
Ni umasikini?
Ni ushamba?
Ni kasumba?
Ni ukosefu wa Exposure? Ama ni nini?
Nashangaa jiji kubwa Kama la DAR mpaka sasa halijaandaa program ya kuukaribisha mwaka mpya Kama majiji mengine makubwa Duniani Kama Dubai, Paris, New York, N.k.
Amani ipo, Jeshi lipo, watu tupo, madini yapo, pesa ipo, nini kinashindikana?
Yaani migodi yote hii tunashindwaje Kula Bata jamani😀😀
Nataka kuziona zile countdowns za kuupokea mwaka mpya kwenye majiji makubwa hapa nchini. Nataka kuona Fataki za kueleweka zile zinazorushwa angani 😀
Sio miji Ipoe Kama uji.
Pesa ipo, tozo tukateni.
Migodi ipo
Mbuga zipo
Watu tupo.
Tunataka tufurahi Sisi, kuzubaa hatutaki.
Umasikini ni pamoja na kuzubaa zubaa kushindwa kufurahia Maisha na kujibana pasipo sababu za maana.
Haya Wahaya jioni nitakuwa kwenu huko!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Mikocheni, Dar es salaam