Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 269
- 332
Ndugu zangu, hapa Mwanza tuna hospitali ya kanda ya Bugando ambayo lengo la uwepo wake ni kuokoamaisha ya Watanzania wa mikoa ya kanda ya Ziwa na mikoa jirani.
Hospitali hii inaaminika kwakua inao watumishi waliobobea kwenye kada zote, na wapo madaktari bingwa kwenye hospitali hii.
Cha kushangaza ni kwamba baadhi ya wagonjwa hufariki kwa uzembe wa kutoa huduma bora kwenye hospitali hii, mfano mwaka 2023 alifariki ndugu yangu aliyekuwa akipewa matibabu kwenye hii hospitali.
Ilikua hivi, alipelekwa bugando ijumaa na kupimwa kipimo kikubwa cha MRI baada ya kupimwa, tukaambiwa wataalamu wa kusoma majibu wako Off kwakua ni wikendi, tukaambiwa jumatatu yake angepewa majibu, isivyo bahati akafariki jumatatu asubuhi hata kabla ya majibu, na wakati wote walikua wakimpa dawa za maumivu, hivyo hii tabia ife mara moja, maana naambiwa sasa imekuwa mwendelezo, kuna mgonjwa yuko hapo tangu ijumaa anasumbuliwa na Moyo saana, mpaka leo hajapewa majibu ya vipimo Tangu ijumaa badala yake wanampa Amoxline ambazo angepata hata mtaani, huyu nae akifa sababu ya kutopewa huduma stahiki TUTASHINDWA KUVUMILIA, Serikali wekeni mkono hapa Waziri wa Afya simama kidete...