Brand za mavazi kama GUCCI, CALVIN KLEIN na VERSACE watanzania hatuzijui au hazitufai?

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,525
15,720
Wakuu Salaam.
Hizo brand hapo juu wana mavazi mengi sana kuanzia viatu, suruali, saa , underwear, kofia na kadhalika , cha ajabu kwa Africa ukitoa Nigeria, south africa, Uganda, egypt maeneo mengi ikiwapo Tanzania naona watu hawajishughulishi na mavazi ya hao jamaa sijui kwa nini?
 
Hizo brands ulizotaja kwa maono yangu naona zinaendandana sana na class ya mtu au watu, angalia nchi ulizomention na watu wake.
 

Tatizo jingine ni serikali yetu kushindwa kusimamia uinguzaji wa bidhaa feki. Kuna feki nyingi zaidi ya genuine za bidhaa hizo kupelekea watu kutukuona umuhimu wa kuzishobokea.
Kingine ni hali yetu ya uchumi majority ni duni, hizo ni expensive products ndio maana feki ni nyingi.
 
WAUZAJI WENGI WAMEINGIA KWENYE BIASHARA KWA KUIGA.
Utakuta muuzaji hajui hata vipimo vya nguo,ukingia dukani anakwambia 'jaribu hii nguo itakufaa'au 'wengi wanapenda hii nunua ukavae'.
Mashariki ya mbali hizo 'brand'zipo ni kwamba wauzaji hawafuatilii ubora bali ili mradi nguo tu.
 
Zinajulikana ila kwa class fulani tuu
 
Mkuu hizo ni Global Brands mara nyingi zipo katika ubora 2wake halisi bei yake ipo juu unakuta Levis Jean inauzwa kwa namba 350,400,550 650 na 700 style zimetofautiana kwa namba kama Lee jean sasa wenzetu wana sale pia katika maduka yao kufanya mzunguko wa hizo brand kuwepo mwingi mtaani...
 
Niliwahi kuishi kinshasa maduka yako mengi na brand shops za kifaransa ziko pale sema bei ndio hatari..
 
Mkuu umenena kweli, yani unaingia dukani alafu unakutana na kika nguo unayoiona ama iko over size ama ndogo.
 
Mchina kesha chakachua, hazina ubora tena..
 
Niliwahi kuishi kinshasa maduka yako mengi na brand shops za kifaransa ziko pale sema bei ndio hatari..
Achana na bei za brand za kifaransa wanazovaa wakongoman ni classic kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…