Boniface Kajunjumile Asinyile Mwabukusi Rais Mpya wa Tanganyika

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
1,049
3,084
Boniface Kajunjumile Asinyile Mwabukusi akianzisha chama chake nje ya vyama vilivyopo vinavyotumia "surname" kwa ajili ya kusurvive akitanguliza maslahi ya Tanganyika basi asubuhi sana Watanganyika watampigia kura ya urais ili kulinda maslahi na rasilimali za Tanganyika,rejea mapambano ya Wakili Mwabukusi kwenye mkataba wa bandari,Umaarufu wake mitaani ni kwa sababu anaonekana yupo tofauti na mamilioni ya Watanzania ambao sifa yao kuu ni unafiki,uongo,uchawa,ufitini na kujipendekeza,wapo watu wengi wanaweza kusema wanafaa kwa urais lakini shida ni kwamba wana tabia asilia za kitanzania za uchawa hivyo hawana public support,

Wakili Boniface Kajunjumile Asinyile Mwabukusi alijitoa kama mtanganyika wakati wa sakata la mkataba wa bandari akaacha kwa muda sifa kitanzania akawa shujaa na lulu kwa Watanganyika maana alionekana ni wa tofauti na Watanzania wengi kama sio wote,niliwahi kusoma mahali waliandika kwa kihaya "The politics of Tanzania is leading the country and has caused generations of Tanzanians to be full of intrigue, hypocrisy, lies and theft in their daily lives,no one is thinking about the wider interests of the country except President John Pombe Magufuli, they are only thinking about their interests and their families Tanzania's people include Generation Z are raised with hypocrisy on what to think not how to think"

Generation Y wamekua "babyface" watu wa kuheshimu watangulizi wetu kuenzi mambo yao na kutenda kufuata utamaduni wa watangulizi wetu,Generation Z wao wamekuja na mfumo tofauti,wao wanataka waanze kazi leo kesho awe Manager,kesho kutwa kanunua ndege anapaa angani,mbaya zaidi Generation Z ya Tanzania wao hawana akili ya kuwaza kesho ya nchi yao,hawana muda na sukari wapo busy kunywa
Visungura, K Vant wakichanganya energy drinks ssubuhi mchana jioni usiku wao wanawaza amapiani shisha udaku umbea dini za miujiza Simba Yanga wakitulia wanawaza teuzi,hata ukiuza bandari ngorongoro migodi BRT Mwendokasi wewe uza tu wao wanataka furaha wakiikosa nyumbani basi watasubiri furaha ya simba na yanga tu baas wao laam starehe wanapata siku mwororo na ubaya ubwela,udugu umala,hawajui tafsiri ya ubaya ubwela udugu umala ni kwamba ubaya umerudi na undugu umeisha kila mtu achukue chake.

Nimalizie kwa kusema Rais mteule wa TLS, Wakili Boniface Kajunjumile Asinyile Mwabukusi atarudisha na kulinda mali za Watanganyika kupitia Tanganyika Law Society,mambo ya kutoa sadaka za rasilimali zetu kwa Waarabu,Wazungu na Wachina kwa jina la uwekezaji sasa limepata muarobaini wake,sasa sadaka tutawapa yatima masikini na Wahitaji ndani ya Tanganyika na hiyo ndio sadaka bora.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom