Boniface Jacob: Chadema kuwapa ushirikiano Polisi ni usaliti na mzaha kwa roho za waliotekwa, kupotea na kuuawa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,664
165,640
Meya mstaafu wa jiji la Dar es Salaam, Boniface Jacob, amesema kuwa alipokea taarifa kwamba Jumanne, tarehe 10 Septemba 2024, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kupitia Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO), liliwasiliana na mawakili wa CHADEMA na kuwaeleza kuwa wanamuhitaji Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, kwa mahojiano.
Screenshot 2024-09-11 161237.png


Nadhani bado ni tetesi 🐼

----
CHADEMA KUWAPA USHIRIKIANO POLISI NI USALITI NA MZAHA KWA ROHO ZA WALIOTEKWA, KUPOTEA NA KUUAWA.

1. Nimetaarifiwa kuwa Jana Jumanne 10 September 2024 jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kupitia RCO Kinondoni waliwapigia simu mawakili wa CHADEMA kwamba wanamuhitaji Katibu Mkuu John Mnyika kwa mahojiano.

2. Kama John Mnyika na CHADEMA watatoa Ushirikiano kwa Jeshi la Polisi Tanzania kufuatia kitu kinaitwa kamati ya uchunguzi watakuwa kuwa wamefanya mzaha mkubwa juu ya sisi wanachama wao tunotekwa, kuuawa na kupotea kwa kukubali kuwapa ushirikiano watuhumiwa namba moja wa matukio hayo.

3. Jeshi la Polisi halina uhalali wa Kimaadili Kufuatia kupotea kwa watu zaidi ya 100 na sita wakiwa ni wanachama wa CHADEMA huku mmoja akiokotwa akiwa ameuawa maeneo ya Ununio

4. Viongozi wa CHADEMA wakae vikaoni watoke na msimamo mmoja wa chama kuhusu wapi watapeleka ushahidi wao na maelezo wanayo yajua kuhusu watekaji na wauaji•Taarifa ambazo CHADEMA wanazo na wana uhakika nazo isipokuwa hawana mamlaka inayoaminika na yenye nia ya dhati ya kushughukikia madai yao.

5. Jeshi la Polisi Tanzania halina mpango wa kuchukua hatua wala kukomesha utekaji na mauaji ya wananchi au makada wa CHADEMA bali wanalenga kutaka kujua CHADEMA wanajua nini kuhusu tuhuma zao ili watumie nafasi hiyo kuficha ukweli na kuharibu ushahidi.

6. Jeshi la Polisi Tanzania lilimsikia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe 22 August 2024 kufuatia tuhuma kwa Jeshi la Polisi, akimtuhumu ZCO Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, ACP FAUSTINE MAFWELE kuhusika katika kuratibu na kusimamia vikundi vinavyoendesha utekaji ndani ya Jeshi la Polisi, wakiwa na makao yao nyuma ya Kituo cha polisi Chang'ombe maarufu kama Tembo 7

7. Jeshi la Polisi pamoja na Kusikia tuhuma za Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe za 22 August 2024, Hawakuwahi kujitokeza hadharani kukanusha tuhuma hizo.•Hawakuwahi kumuhitaji Freeman Mbowe kumuhoji na kutaka kujua ukweli wa tuhuma hizo. •Hawakuwahi kumfungulia mashtaka Freeman Mbowe juu ya upotoshaji au uchochezi kama tulivyo wazoea.•Hawakuwahi kuhabarisha umma kuwa tuhuma za Freeman Mbowe zilikuwa zinafanyiwa kazi.

8. Jeshi la Polisi Tanzania walichofanya ni kwenda kuvunja maskani ya kikosi kazi kinachotuhumiwa na Freeman Mbowe, kuendesha shughuli za utekaji na mauaji nyuma ya kituo cha Polisi Chang'ombe maarufu kama "TEMBO 7" na sasa wamehamia sehemu mpya ya maeneo ya Mpingo House.•Huku askari waliotajwa na Freeman Mbowe walifuta akaunti zao katika mitandao ya kijamii kama alivyofanya Afande Semageni Shabani mmoja wa watuhumiwa katika kikosi kazi cha Polisi Chang'ombe (Tembo 7)

9. Kama Jeshi la Polisi Tanzania wangekuwa wana nia ya dhati ya kushughulikiia tuhuma za Mwenyekiti wa CHADEMA huenda Kifo cha Kiongozi wake wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa Bwana Ali Muhammad Kibao kisingetokea.

10. Tarehe 07 September 2024 majira ya Saa 6: 00 mchana, Wakati Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika anafamya kikao na Waandishi wa Habari kulitaka Jeshi la Polisi lijitokeze kusema alipo Kiongozi wake Ali Muhammad Kibao •Tayari Jeshi la Polisi lilikuwa limeshauchukua Mwili wa Ali Muhammad Kibao kutoka Ununio na kupeleka hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala•Siku hiyo tarehe 07 September 2024 Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime akitoa taarifa yake kuhusu kufanyia kazi tuhuma za John Mnyika tayari Jeshi la Polisi ilikuwa limeshaokota Mwili wa Ali Muhammad Kibao kwa zaidi ya saa 8 zilizopita tangu saa 1:00 Asubuhi baada ya Wakulima wa mchicha wa Ununio kujulisha mamlaka kuhusu kukutwa kwa mwili wa binadamu eneo la jirani la vitalu vyao vya mchicha.

11. Wakati wote huo Jeshi la Polisi lilikuwa linajua Mwili huo uliookotwa eneo la Ununio ndiyo Mwili wa Kiongozi wa CHADEMA anayetafutwa.

• Badala ya jeshi la Polisi Kuwajulisha CHADEMA wao waliwazunguka CHADEMA na kuwatafuta ndugu wa Marehemu Ali Muhammad Kibao na kuwataarifu wafike hospitali ya Mwananyamala siku hiyo hiyo ya Tarehe 07 September 2024 majira ya mchana.

• Na hata ndugu walipoutambua mwili wa marehemu Ali Muhammad Kibao Jeshi la Polisi lilificha taarifa isiwafikie CHADEMA na kuwaomba Wanafamilia Msiba uwe siri na usiwe wa kisiasa kwa kuwaondoa CHADEMA wasiwe sehemu ya msiba. Na hata CHADEMA na mawakili wao walipofika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala sehemu ya kuhifadhia maiti polisi waliwazuia CHADEMA kuingia ndani ya chumba cha Autopsy

• Hii pia inathibitishwa na taarifa ya Jeshi la Polisi ya tarehe 07 September 2024 kupitia kwa Msemaji wake DCP David Misime ambapo alisema kuwa wapo tayari kushirikiana na familia tu huku wakikwepa kutaja CHADEMA katika taarifa yao pamoja na kujua marehemu ni Kiongozi wa CHADEMA

• Je, leo Jeshi la Polisi ndiyo limegundua linahitaji Ushirikiano na CHADEMA? Huu kwa lugha rahisi tu, tunaweza kuita ni unafiki wa kiwango cha juu sana na hatutakiwi kuufumbia macho.

11. kuanza kutafutwa leo na Jeshi la Polisi ni unafiki mkubwa. Jeshi la Polisi liliwapuuza CHADEMA likaziba masikio na kuacha kufanyia kazi tuhuma za CHADEMA kwa askari wake wanaotajwa kuendesha Operesheni za kuteka na kuua watu. Badala yake watuhumiwa hao wapo maofisini wanaendelea na kazi chafu wanazotuhumiwa nazo.Baada ya kuona Rais Samia anatoa pole kwa familia na CHADEMA na Kulaani mauaji ndiyo Jeshi la Polisi likaanza kujifanya linafanya uchunguzi au kuongeza Polisi Wengine kuchunguza tukio la kutekwa Ali Kibao na kuuwawa.

12. CHADEMA wasiingie katika mtego huo wa kuhojiwa na Polisi tena na RCO ambaye yupo chini ya Usimamizi wa Boss wake ZCO Faustine Mafwele ambaye CHADEMA wamemtuhumu hadharani kuhusika na mutekwa na Kupotea kwa watu Dar es saalam ikiwemo Godwin Mlay, Deusdedith Soka na Frank Mbise. Badala yake CHADEMA waandae ushahidi na mashahidi wao kwenda kutoa taarifa na maelezo kwa tume huru ya kijaji kama ilivyokuwa kwa Jaji Kipenka Mussa katika mauaji ya Wafanyabiashara wa Mahenge, Morogoro itakayokuwa huru kukusanya taarifa, kuhoji wahusika na mashahidi pamoja na kutoa mapendekezo juu ya kila tuhuma za mtuhumiwa.

Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
The voice of the silenced Majority

 
Mayor DSM Mstaafu Boniface Jacob amesema ukurasani X kwamba ametaarifiwa Kuwa Katibu mkuu wa Chadema Mh Mnyika anahitajika police Kinondoni

Boniyai anasema Mawakili wa Chadema walipigiwa simu jana na RCO ya kumuhitaji Mnyika kituoni

Nadhani bado ni tetesi
Hao makoboko yanataka yambambikizie kesi kuhusu tamko la kifo cha mzee wetu
 
Back
Top Bottom