Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,106
- 10,178
NAPE KALIDANGANYA BUNGE KUHUSU ELIMU YAKE
Katika kufanya Utafiti wangu kuhusu mapitio (background) ya elimu ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Bw. Nape Moses Nnauye nimeshtuka kuona Bunge linatangaza Waziri Nape Moses Nnauye amepata Elimu ya Advanced Certificate of Secondary School katika shule ya Butimba TTC mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
Nimelazimika kuwatafuta Walimu wenzangu waliosoma na kufanya kazi Butimba TCC (Butimba teacher's college).
Wameshangaa na kushtushwa na taarifa ya Bunge inayohusu elimu ya Waziri Nape Moses Nnauye.
Ukweli ni kwamba Butimba TCC haijawahi kuwa na shule ya Sekondari mwaka 1998 wala katika tovuti ya Baraza la Mitihani Tanzania halijawahi kusajili Shule ya Sekondari na kuipa mitihani mwaka 1998 hadi 2000 kwa Jina la "Butimba TCC Secondary School".
Butimba TCC (Butimba teacher's college) ilianzishwa mwaka 1939 na wakoloni na kujengwa shule ya msingi ya mazoezi (Teaching Practice) na wakoloni wenyewe kwa ajili ya mafunzo kwa Vitendo kwa Wanafunzi wa Ualimu.
Hata hivyo 28 January 2000 serikali ilianzisha shule mpya ya sekondari (kutwa) ya Butimba Secondary School (Butimba Day) ambayo kidato cha kwanza waliingia mwaka 2000 na kumaliza mwaka 2003 kidato cha nne.
Ambapo kwa mujibu wa tovuti ya Bunge, Nape alikuwa ameshamaliza kidato cha 6 mwaka 2000 latika Shule ya Sekondari ya Butimba TCC.
Lakini kubwa zaidi inaonyesha Nape Moses Nnauye hakusoma Butimba TCC elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne bali alisoma kidato cha tano na cha sita katika Shule ambayo haipo wala haijawahi kuwepo.
Pichani ni tovuti ya Bunge kuhusu elimu ya Nape Moses Nnauye, picha ya pili ni kuhusu usajili wa Sekondari wa Butimba Day mwaka 2000.
Naomba kuwasilisha.
Namalizia utafiti kuhusu Shahada ya Sheria pale Open University of Tanzania anayosoma Nape Moses Nnauye.
Imewezekanaje mwanafunzi aliyekosa qualificayion za direct entry za;
1. "Principal mbili" za Advanced Certificate of Secondary School?
2. Credit mbili za O-level (History na English language)
(Inawezekanaje mwanafunzi huyo) kusoma Sheria kinyume na Kanuni za TCU?
3. Au mwanafunzi aliyekosa Equivalent qualifications za Diploma yenye G.P.A yenye 3.0 and above anawezaje kujiunga na Shahada ya Sheria? Au mtafuta kuwapa lawama Law School Tanzania
Kaka ana madiploma mengiiiiiiiii lakini hayana uzito!
4. Au Bachelor degree kutoka Chuo kinachotambulika na TCU, siyo kama Bangalore Universitu of India? 😂😂😂
La sivyo TCU mtuambie mtu akiwa CCM au Kiongozi wa Serikali Vigezo vya kujiunga na elimu ya juu kwake havizingatiwi sawa na Watanzania wengine?