Boniface Jacob afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,665
239,156
Boniface Jacob tayari amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Ni jioni ya leo Alhamisi, Septemba 19, 2024 na anasubiri hakimu aingie mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Jopo la waendesha mashtaka mawakili wa Serikali wakiongozwa Job Mrema pamoja na jopo la mawakili wa Jacob linaloongozwa na Peter Kibatala wapo ndani ya ukumbi wa mahakama sambamba na wanachama wa Chadema.

Boni Yai alikamatwa jana Jumatano, maeneo ya Sinza na Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Osterbay. Kisha usiku wa jana alipelekwa nyumbani kwake Mbezi Msakuzi kwa upekuzi.
boni yai.jpg

Boniface Jacob akiteta jambo na Wakili Kibata katika Mahakama ya Kisutu
Haijafahamika kama amesomewa Mashtaka au la, Na wala Mashtaka aliyosomewa hayajulikani

Usiondoke JF kwa Taarifa zaidi

Soma, pia: Boniface Jacob adaiwa kukamatwa na watu waliokuja na gari aina ya defender. Kamanda Kitwinkwi asema hana taarifa hizo
 
Wakati mwengine hizi nchi zetu za Kiafrika maskini choka mbaya zinachekesha sana,tuna viongozi wapumbavu mbumbumbu waliokosa vision na bado wanateuwa watu wa hovyo sana mfano

Vurugu zote hizi magari yanawekwa mafuta watu wanasaini posho kufanya huu ujinga na wanajua kabisa at the end of the day hakuna kitakachotokea zaidi watakuwa wamepoteza muda na gharama source ikiwa ni kodi za wananchi walizojiaminisha kwao kwamba watazisimamia kuwapelekea maendeleo.
 
At least tungekuwa tunapelekana Mahakamani na kupeana taarifa kwanini tunakamatwa huenda wala kungekuwa hakuna sintofahamu wala kushutumiana....

 
Back
Top Bottom