Bondia Mandoka achapika, Kidunda ashinda, Mapambano ya ndondi Uwanja wa Majimaji - Songea, Julai 30, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,696
6,491
Tayari mapambano yameshaanza ulingoni ndani ya Uwanja wa Majimaji Mjini Songea, leo Jumamosi Julai 30, 2022:

Usungu Ndunguru  (2).jpg

Ndunguru ashinda
Bondia Usungu Ndunguru amefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Bernard Chitepete katika pambano la awali. Wamepigana uzito wa Super Light, raundi 6.

Mtu kachapika TKO Mapema tu
Ezra Paul amefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Kassim Gambo kwa TKO katika raundi ya kwanza, Ezra alianza mchezo kwa kasi akawa anampelekea ngumi mfululizo mpinzani wake, licha ya kujibu lakini zilipozidi akapiga goti chini, alipohesabiwa na mwamuzi hadi 10 akashindwa kuendelea.

Lilikuwa pambano la Raundi 6 uzito wa Super Light.

Chokoraa.jpg
Chokoraa apigana, matokeo sare
Khalidi Chokoraa na Chidi Benga wamepata matokeo ya sare baada ya raundi nne kukamilika. Lilikuwa ni pambano la Super Welter. Chokoraa alianza vizuri akaonekana kuchoka kadiri raundi zilivyokuwa zinaenda mbele.

Alitumia mbinu ya kumbana mpinzani wake mara kadhaa huku akipata sekunde kadhaa za kuvuta pumzi.

Grace Mwakaele ashinda kwa KO
Grace Mwakaele amepata ushindi wa KO katika Raundi ya Pili dhidi ya Suzana Mahenge. Lilikuwa pambano la uzito wa Super Light.

Musa Chitepe ashinda kwa pointi
Musa Chitepe na Salvatory Urio wamepigana katika pambano la Super Welter la Raundi 6, Chitepe amefanikiwa kupata ushindi wa pointi, amecheza vizuri na kutawala asilimia kubwa ya mchezo huo licha ya kuwa mpinzani wake pia alikuwa makini na kujibu mashambulizi mara chache.

Pambano la Habibu Pengo lasitishwa
Habibu Pengo alitakiwa kupigana na Said Mkola lakini pambano limefutwa bada ya Mkola kupata majeraha ya kuumia katika guu wa kulia. Alionekana akichechemea na kushindwa kupanda ulingoni.

Pengo amehojiwa na kuonesha kuwa na hasira kali, akizungumza huku akilia amesema anaamini mpinzani wake hajaumia bali kamkimbia.

George Bonabucha amchakaza Yusuf Ali
Pambano la Uzito wa Super Bantam la Raundi 6 kati ya George Bonabucha dhidi ya Yusuf Ali limekuwa kali muda mrefu, ushindani ni mkubwa, zimepigwa ndoga hasa. Bonabucha ameshinda kwa pointi.

Ismail Galiatano ashinda
Ismail Galiatano ameshinda kwa TKO baada ya mpinzani wake kunyoosha mikono akimaanisha ameshindwa kuendelea katika pambano la Uzito wa Light.

Mandonga achapika
Karim Mandonga amepoteza dhidi ya Shabani Kaoneka katika pambano la Uzito wa Super Middle, amepoteza katika Raundi ya 4, alipata makonde kadhaa akaonekana kupoteza mwelekeo.

Mwamuzi akalazimika kuingilia kati na kumuokoa. Baada ya pambano Mandonga amesema kilichotokea ni ajali kazini.
FY8NbDcWQAACcbZ.jpg

FY8JO-0WQAEpICp.jpg

Kidunda amdunda Eric Katompa wa DRC
Bondia Mtanzania Selemani Kidunda amefanikiwa kumpiga Eric Katompa wa DRC kwa pointi katika pambano la uzani wa Super Middleweight Raundi 10.

Kwa ushindi huo Kidunda amefanikiwa kuchukua Mkanda wa WBF Inter Continental ambapo alitawala sehemu kubwa ya pambano hilo licha ya mpinzani wake kutoa upinzani mkali katika Raundi ya 7 na 8.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom