Pre GE2025 Bombambili Songea: Mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF). Mgeni Rasmi ni KM wa CCM Taifa, Dkt. Emmanuel Nchimbi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Muulize maswali ya msingi basi badala ya kuuliza maswali ya kujipendekeza tu. Sijui ni kwa nini wahariri na waandishi wa habari wa sasa mko tofauti kabisa na wale wa zamani kama Tido Mhando. Mko na njaa sana siku hizi.
 
Nchimbi. Kati ya viongozi waliopikwa wakapikika. Ila sasa sisiemu ya leo imeacha misingi ya siasa za kistaarabu na yeye lazima afuate mkumbo huohuo. Siku hizi domo lako tu linakupa vyeo kedekede.... Hasa ukijua kutukana.
 
Muulize maswali ya msingi basi badala ya kuuliza maswali ya kujipendekeza tu. Sijui ni kwa nini wahariri na waandishi wa habari wa sasa mko tofauti kabisa na wale wa zamani kama Tido Mhando. Mko na njaa sana siku hizi.
Sio kila mkutano wa Wahariri ni press conference, hivyo unadhani Dr. Nchimbi yuko hapa kwa ajili ya kuulizwa maswali!, kumbe masikini hujui kuwa huu ni mkutano Mkuu Maalum wa TET na sio Press Conference.
P
 
Jukwaa la Wahariri ni moja ya project za Chama cha Mapinduzi katika kuwarubuni Watanzania na kuendelea kuwafanya wajinga.

Msitegemee chochote kutoka kwenye hicho kikao. Hapo utakuta Wahariri wote wamelipwa posho na kupewa fedha za malazi na CCM alafu mnategemea cha tofauti?

Kalaghabao!!!
 
Yameenda kukusanywa Songea yaani hayana akili kabisa kwenda kujipendekeza, hizi ni project za CCM
 
Sio kila mkutano wa Wahariri ni press conference, hivyo unadhani Dr. Nchimbi yuko hapa kwa ajili ya kuulizwa maswali!, kumbe masikini hujui kuwa huu ni mkutano Mkuu Maalum wa TET na sio Press Conference.
P
Sawa Comrade. Nimekuelewa.
Ila ni vizuri pia mngetoa sababu ya msingi ya kumualika mgombea umakamu wa Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025, kwenye Mkutano wenu mkuu maalum wa TET!

Labda mngemualika Waziri mwenye dhamana kwenye masuala ya habari, walau kidogo mngeeleweka. Why Dr. Emmanuel Nchimbi, mgombea mwenza kupitia ccm 2025?
 
Back
Top Bottom