The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 742
- 1,192
Mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Paul Makanza, ameongoza ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa kituo mama cha ujazaji gesi asilia kilichopo Mlimani, Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Akizungumza leo Jumatatu, Machi 3, 2025 mara baada ya ziara hiyo, Makanza amesema mradi huo ni muhimu kwa sababu gesi asilia iliyokandamizwa (CNG) ni mbadala wa mafuta, hatua inayosaidia nchi kuokoa fedha za kigeni na kuboresha uchumi.
"Tumeridhika kama Bodi kwa maendeleo ya mradi huu. Unapokuwa mkubwa, faida zake zitakuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa kwa kupunguza utegemezi wa mafuta ya petroli," amesema Makanza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa TPDC, Derick Moshi amesema kituo hicho kimekamilika kwa zaidi ya asilimia 90, huku hatua za mwisho zikiwa ni ukaguzi wa usalama kabla ya kuanza majaribio rasmi.
"Kituo kimeshakamilika kwa kiwango kikubwa, na gesi tayari ipo. Tunachosubiri kwa sasa ni majaribio kwa magari. Tunatarajia kabla ya mwisho wa mwezi huu kila kitu kitakuwa tayari," amesema.
Mradi wa kituo mama cha ujazaji gesi cha Mlimani ni sehemu ya juhudi za serikali katika kukuza matumizi ya nishati mbadala na kupunguza gharama za uendeshaji kwa watumiaji wa magari yanayotumia gesi badala ya petroli au dizeli.