kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,946
- 14,518
Bodi ya ligi inahanyahanya iseme nini baada ya kuamrishwa na Simba ifute mechi ya derby. Kama takukuru ingethibitisha kuwa Yanga imetoa rushwa kwa yeyote ili kushinda mechi bado bodi ya ligi ingeweza kutumia ushahidi huo wa TAKUKURU kuipoka Yanga points 3 na kuipa Simba, lakini sio kuahirisha mechi masaa 3 kabla ya mechi kwa dhana na tetesi tu. Jeshi la polisi walisema walijipanga kikamilifu kwa mchezo wa derby tarehe 8 kudumisha usalama kabla, wakati na baada ya mechi, nani kasema derby isingekuwa salama? isingekuwa salama kwa nani, wachezaji, waamuzi, viongozi wa bodi au kwa mashabiki wa timu ipi? ni utetezi wa mfa maji tu. Maanda huwezi kuhukumu jambo kubwa kama lile ililiandaliwa kwa miezi mingi kwa kutumia tetesi na hisia masaa 3 kabla ya mechi; ni uhuni wa kishamba kabisa.
Baada ya Simba kufungwa magoli 5-1 na Yanga, simba waliwatuhumu akina Aishi Manula na wenzake kuwa walikula rushwa Simba ifungwe; mbona bodi ya ligi na TFF haikufanya uchunguzi wa tuhuma hizo nzito? Mwamuzi Smart alimpa red card mchezaji Mukombozi na kadi hiyo ikafutwa kuwa ilitolewa kinazi, mbona bodi ya ligi na TFF hawakufanya uchunguzi kwanini jambo lile lilitokea? Why derby?