the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 498
- 722
Taifa lina utani sana hili yani watu wenye matatizo wananmchangia mtu mwenye pesa akaendelee kuzichota pesa. Na hawa wamefanya hivi kwa sababu hiyo maboboda yenyewe wamepewa na Tulia huyo huyo
===
Leo tarehe 4 Machi, 2025 Umoja wa Madereva wa bodaboda Mbeya Mjini umemwomba Mbunge wa jimbo hilo, Dkt. Tulia Ackson, kugombea tena katika uchaguzi wa 2025 kutokana na utendaji wake mzuri. Katika kuthibitisha dhamira yao, wamechangia shilingi milioni moja kama mchango wa kuchukua fomu ya kugombea.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ofisi zao Kata ya Ilolo, mwenyekiti wao, Aliko Fwanda ambaye pia ni kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema kuwa maendeleo hayana itikadi na wanahitaji Dkt. Tulia amalizie kazi aliyoianza.
Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa upande wake, Dkt. Tulia amewashukuru na kuwaahidi kuendelea kuwatumikia kwa bidii. Pia amewataka wananchi kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Oktoba 2025 ili aendeleze maendeleo nchini.