adakiss23
JF-Expert Member
- Jan 23, 2011
- 4,652
- 4,692
Inasikitisha sana uwapo katika makutano ya barabara pale ambapo waendesha pikipiki wanavyotawala dunia yao ya sheria za barabarani. Si salama kabisa kwa watumiaji wengine wa barabara ie wenye magari, watembea kwa miguu nk.
Eneo kama Tazara ni eneo la hatari sana. BodaBoda hawafuati sheria kabisa. Mfano taa zimeruhusu upande mmoja lakini BodaBoda wao wanakwenda kama wendawazimu kila upande. Nmeshuhudia ajali zaidi ya 4 kwa aina hiyo hiyo ya makosa. BodaBoda kugonga gari, mtembea kwa mguu ambao wapo ktk eneo salama kwa kuwa taa zimewaruhusu kufanya hivyo.
Nashangaa eneo lile kuwa na Askari Masai 24 lakini wanazidi kufumbia macho suala hili la hatari au mpaka itokee ajali kubwa itakayohusisha kundi kubwa la watu ndio tuchukue hatua? Ikumbukwe watumiaji ni wengi na sio wote wenye elimu kubwa ya matumizi ya barabara. So anapovuka anapoona ni sahihi kwake (in most cases yes) utakuta BodaBoda anapita eneo hilohilo pasipo kuruhusiwa kufanya hivyo.
Hakuna tena utaratibu ni vurugu mechi, kila mmoja kutembea au kuendesha kwa timing tu. Hii ni hatari maana kuna wazee watoto walemavu wagonjwa nk.
Mbona nchi ambazo kuna aina hii ya usafiri utaratibu unafuatwa vizuri tu. Mathalani mji kama Kampala ambao BodaBoda ni nyingi lakini taa au askari akiruhusu upande mmoja ni magari baskeli BodaBoda za upande huo tu utahusika hapo. Tofauti na hapa kwetu kabisa.
Serikali chukueni hatua haraka mno.